Hali inaonekana kuwa si shwari kihivyo ndani ya klabu ya Yanga, hasa
baada ya mashabiki wa klabu hiyo kumshambulia beki Vincent Bossou
mtandaoni.
Mashabiki wa Yanga wanaonyesha kuchukizwa na Bossou kutokana na uamuzi wake wa kutotaka kucheza katika kikosi hicho.
Taarifa zinaeleza Bossou amegoma kucheza kwa kuwa anadai mshahara wake wa miezi kadhaa.
Lakini kupitia mtandao wa Instagram, Bossou amesema anaidai Yanga mshahara wa miezi minne.
Ingawa Bossou Kingereza chake ni cha "kuunga" amewajibu mashabiki wa
Yanga, kwamba yuko tayari kuondoka ila wamlipe mshahara wake wa miezi
minne.
Beki huyo raia wa Togo, tayari ametishia kuondoka Yanga, hali
inayoonyesha mambo hayajakaa vizuri kwa kuwa mshambuliaji Donald Ngoma
naye amekuwa akielezwa kuwa mgonjwa lakini kuna taarifa kuwa anafanya
mgomo baridi.
No comments:
Post a Comment