Mahakama ya Rufaa nchini imetupilia mbali rufaa ya kupinga hukumu ya
kesi ya uchaguzi katika jimbo la Longido mkoani Arusha, yaliyompa
ushindi Onesmo Ole Nangole (Chadema), iliyofunguliwa na aliyekuwa
mgombea wa CCM, Dk. Stephen Kiruswa,
Uamuzi huo umesomwa leo (Alhamisi) na msajili wa Mahakama ya Rufaa
nchini, Amir Msumi na kusema kwamba wakata rufaa waliwasilisha rufaa
mpya badala ya kurekebisha baadhi ya vipengele kama walivyoagizwa na
mahakama.
Msumi amesema badala ya kuwajumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na
msimamizi wa uchaguzi kwenye rufaa hiyo, wakata rufaa walifanya kitu
ambacho hawakuruhusiwa kukifanya na mahakama na hivyo rufaa hiyo
imetupwa na wanapaswa kulipa gharama za uendeshaji wa kesi hiyo.
No comments:
Post a Comment