Saturday, 25 February 2017

Askari Polisi 350 katika mchezo wa Simba na Yanga

Askari Polisi wapatao 350 watamwagwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi kulinda usalama wakati Simba na Yanga zikipambana katika mchezo namba 169 wa Ligi Kuu Bara.
Askari hao watakuwa wakilinda usalama wa ndani na nje ya uwanja huo uliopo Manispaa ya Temeke na mtu yeyote atakayefanya fujo au uharibifu ataishia mikononi mwao.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesema, askari hao watashirikiana na watu wengine kutoka majeshi mengine na kampuni binafsi za ulinzi kuhakikisha usalama unatawala uwanjani hapo.
“Kuna polisi 350 ambao leo  watafanya mazoezi uwanjani wakijipanga kwa ajili ya kulinda kesho (leo) kuhakikisha hakuna vurugu au uhalifu wowote utakaotokea.



“Nawasihi wote watakaofika uwanjani kutazama mechi kwa utulivu na kutofuata mkumbo wa kufanya fujo kwani wataishia mikononi mwa polisi na walinzi wengine wa siri.
“Hatuwezi kukubali kuona watu wanajipanga kuharibu miundombinu ya uwanja ambao tulipata tabu kuomba uruhusiwe kwa timu hizi, nawasihi watu wasifanye vurugu,” amesema Lucas.

No comments:

Post a Comment