Waziri wa elimu sayansi na
teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kushoto akiwa na na Mbunge wa Jimbo
la Rufiji wa kulia Mohamed Mchengerwa akizungumza na walimu pamoja na
wanafunzi wa shule ya sekondari Utete wakati wa ziara yake ya kikazi kwa
ajili ya kujionea chanagamoto mbazi mbali zinazoikabili sekta ya elimu.
Waziri wa elimu Sayansi na
teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kulia akiwa na baadhi ya viongozi wa
halmashauri ya Wilaya ya Rufiji mara baada ya kufanya ziara yake ya
kikazi ya kutembelea shule mbali mbali zilizopo Wilayani Rufiji.
Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed
Mchengerwa aliyesimama akizungumza na walimu wa shule ya sekondari ya
Ikwiriri pamoja na walimu wa shule za msingi hawapo pichani,kushoto
kwake ni Waziri wa Elimu wa sayansi na Tekonolojia katika ziara hiyo.
Baadhi ya viongozi wa halmashauri
ya Wilaya ya Rufiji wakiwa katika shule ya sekondari ya Ikwiriri
wakiteta jambo na Wazairi wa elimu sayansi ya na Tekonolojia Professa
Joyce Ndalichako aliyefanya ziara yake ya kutembelea shule mbali mbali
Wilaya hiyo.
NA VICTOR MASANGU, RUFIJI
Shule za sekondari hapa nchini
bado zinakabiliwa na changamoto sugu ya kuwepo kwa upungufu mkubwa wa
walimu wa masomo ya sayansi pamoja na kutokuwa na vifaa vya maabara
kunachangia kwa kiasi kikubwa kushuka na kuzolota kwa kiwango cha
ufaulu kwa wanafunzi kutokana na kufanya vibaya katika mitihani yao ya
kumaliza kidato cha nne na sita.
Katika kuliona hilo Waziri wa
elimu sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako alisema kwamba
serikali ya awamu ya tano kwa sasa imeshaanza kufanya mchakato kwa ajili
ya kuweza kuanza kusambaza vifaa vya maabara katika shule zipatazo 1625
sambamba na kuwaajiri walimu wa masomo ya sayansi wapatao 4200 ambao
wataweza kuleta mabadiliko chanya katika kuongeza kasi ya ufundushashi.
Waziri Ndalichoko aliyasema hayo
wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani
ambapo aliweza kutembelea katika shule tatu za sekondari ikiwemo shule
ya Utete,Muhoro pamoja nna Ikwiriri kwa lengo la kuweza kujionea
chagamoto zinazowakabili wanafunzi pamoja na walimu ili kuweza
kuzitatutia ufumbuzi wa kudumu.
“Ni kweli changamoto hii ipo ya
uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi pamoja na vifaa vya maabara lakini
nipende kuwaahidi kuwa serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta
ya elimu kwa sasa ipo katika mchakato wa kuana utekeleaji wa kusambaa
vifaa vya maabara katika shule 1625 pamoja na kuajri walimu wengine
hivyo kwa Wilaya ya Rufiji msiwe na shaka kabisa katika hili,”alisema
Ndalichako.
Aidha Prosefa Ndalichako alisema
kuwa mchakato huo amabao unatarajiwa kuanza rasmi mwezi wa tatu mwaka
huu pia utazigusa na baadhi ya shule za sekondari zilizzopo katika
halamashauri ya Wilaya ya Rufiji ili kuweza kuondokana kabisa na hali
hiyo na kuweza kuwapa fursa wanafunzi waweze kufanya vizuri katika
mitihani yao bila ya kuwa na vikwazo vyovyote vile.
Aidha Waziri huyo katika hatua
nyingine alipiga marufuku kwa wanafunzi wenye tabia ya kuamua kwenda
kukesha katika ngoma za usiku au kwenda disco na badala yake sasa
amewataka wahakikishe kwamba wanajikita zaidi katika kuongeza juhudi na
mahalifa katika masomo yao ili kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma
katika shule ya sekondari Utete akiwemo Salum Salum pamoja na Sarafina
Muhina walisema kwamba kwa sasa wanajikuta wanasoma katika mazingira
magumu kutokana na kutokuwa na walimu wa sayansi pamoja na vifaa vya
maabara hivyo kuwasababishia kufanya vibaya katika masomo yao tofauti
na matarajio yao.
Pia waliiomba serikali kuweza
kuharakisha zoezi hilo la kuwaajiri walimu pamoaj na kugawa vifaa kwa
ajili ya maabara ili kuweza kuwafanya kuongeza juhudi katika masomo yao
na kulet mabadiliko ya kuongeza kiwango cha ufaulu katika siku za
usoni.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la
Rufiji Mohamed Mchengerwa amebainisha kuwa sekta ya elimu bado ni
tatizo kubwa katika shule za msingi na sekondari hivyo amemwomba Waziri
kulivalia njuga suala hilo kwa kuboresha miundombinu ya madarasa, vyoo,
pamoja na kuongeza idadi walimu ili kuweza kuwapa fursa wanafunzi
wawze kujisomea katika mazingira ambayo ni rafiki kwao.
Pia Mchengerwa alisema kwamba
katika jimbo lake shule nyingi za sekondari zinakabiliwa hivyo
ataendelea kushirikiana na serikali iliyopo madarakani katika
kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri kwa lengo la
kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hao.
KUSHUKA kwa kiwango cha elimu
hapa nchini kwa wanafunzi wa shule za sekondari wanaosoma hususan
masomo ya sayansi kunatokana na kutokuwa na vifaa vya maabara kwa
ajili ya kufundishia kwa njia ya vitendo pamoja na uhaba wa walimu.
No comments:
Post a Comment