SHIRIKISHO
la Riadha Tanzania (RT), limekamilisha hatua ya kwanza na ya muhimu ya
maandalizi ya kuelekea Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika ‘World Cross
Country’ zitakazofanyika Kampala Uganda Machi 26, Mwaka huu.
Jumamosi,
Februari 18 RT iliendesha Mashindano ya Taifa ya Mbio za Nyika katika
Viwanja vya Gofu mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na kushirikisha mikoa
zaidi ya 11 Tanzania Bara na Visiwani, ambapo wakongwe wengi wa riadha
wamekiri kwamba mwamko waliouona juzi haujatokea tangu mwaka 1991 kwenye
mashindano yaliyofanyika Arusha eneo la Mushono.
Mwaka
huo wa 1991, ndiyo mwaka ambao mtanzania pekee Andrew Sambu alishinda
mashindano ya Junior ya Dunia Antwerp Belgium, kwa mfano huo sisi
Shirikisho la Riadha Tanzania tuna imani kubwa na timu iliyochaguliwa
mwaka huu, tunakwenda Uganda kifua mbele, hatuogopi chochote, mataifa
mengine nayo yanafahamu kwamba watanzania wameamua safari hii.
Kwa
vile wengi wenu mlikuwa kwenye tukio juzi, au mathalan habari zote
mnazo; napenda sasa nitangaze majina ya wanariadha waliochaguliwa kwenda
kusaka medali Uganda na kupeperusha vyema bendera yetu.
Waliochaguliwa kwenye timu ya Taifa kwenda Kampala ni wafuatao:
Wanaume Senior 10KM;
1) Emmanuel Giniki – Manyara
2) Basil John – CCP / Kilimanjaro
3) Gabriel Geay – JKT / Arusha
4) Fabian Joseph – Arusha
5) Wilbado Peter – CCP / Kilimanjaro
6) Josephat Joshua – CCP / Kilimanjaro
Wanawake Senior 10KM;
1) Magdalena Shauri – JKT / Arusha
2) Angelina Tsere – JKT / Arusha
3) Failuna Abdi – Arusha
4) Sara Ramadhani – Arusha
5) Jackline Sakilu – JWTZ / Arusha
6) Siata Kalinga – JWTZ / Arusha
Wanaume Junior 8KM;
1) Francis Dambel – Manyara
2) Yohana Elisante – JKT / Arusha
3) Ramadhani Juma – Arusha
4) Elisha Wema – Arusha
5) Anthony Wema – Arusha
6) Joshua Elisante – Arusha
Wanawake Junior 6KM;
1) Cecilia Ginoka – JKT / Arusha
2) Maicelina Issa – JKT / Arusha
3) Asha Salum – JKT / Arusha
4) Noela Remy – Manyara
5) Elizabeth Boniface – Singida
6) Amina Mgoo – JKT / Arusha
Timu ya Relay Wanaume wawili;
1) Faraja Damas – JKT / Arusha
2) Marco Sylvester – Singida
Timu ya Relay Wanawake wawili, itangazwa hivi karibuni kutokana na sababu za kiufundi.
Makocha wa timu ya taifa;
Kamati ya Ufundi ya RT, imewapendekeza wafuatao kuwa makocha wa timu hii ya Taifa.
1) Naasi Gwagwe Dengwe – CCP
2) Thomas John Tlanka– Arusha
3) Francis Nade – Manyara
4) Zakaria Barie – Arusha
5) Lwiza John – Mbeya
Kwanza
nawapongeza Viongozi wakuu wa RT nikianza na Rais wa Shirikisho Mh.
Anthony Mtaka kwa maono yake, bidii za kutafuta namna yoyote ya
kuendeleza mchezo wa riadha, suala la kutoa zawadi kwa washindi katika
mashindano ya mwaka huu ni wazo lake na ndiyo hali iliyoleta hamasa
zaidi.
Pia
suala la kuendesha mashindano mikoani kikanda, pia ni wazo lake, sisi
wengine tuliweka ‘strategies’ ili ‘idea’ ile ikae kiufundi zaidi.
Pia
kwa uamuzi wake wa kipekee, kuamua kuwalipia ada ya ushiriki wa mbio za
Kilimanjaro Marathon, wanariadha wote walioshiriki mbio za Nyika za
Taifa kwa categories zote na kushika nafasi kumi za juu.
Napenda
pia kuwashukuru Makamu wa Kwanza wa Rais RT ambaye pia ni Mwenyekiti
Kamati ya Fedha, Ndg. William Kallaghe kwa kufanikisha
‘Transaction’/pesa mapema, Makamu wa Pili wa Rais ambaye pia ni
Mwenyekiti Kamati ya Ufundi, Dk. Ahmad Ndee kwa kusimamia taratibu zote
za kiufundi, Mama Rehema Killo (Katibu Kamati ya Ufundi), kwa kusimamia
‘logistics’ zote za kiufundi.
Bila
kumsahau Mwenyekiti Kamati ya Mbio za Nyika na Barabara (CC &RR)
Ndg. Meta Petro, Tullo Chambo – Mjumbe wa Kamati Tendaji na Mwenyekiti
Kamati ya Habari na Mahusiano, wanariadha wakongwe wa zamani Zakaria
Barie, Lwiza John, Robert Kalyahe ambao Wajumbe wa Kamati Tendaji na pia
ni wajumbe wa Kamati ya Ufundi, ambao walijitolea kufanya kazi kwa
bidii hadi kikaeleweka, wakishirikiana kwa karibu na Chama cha Riadha
Mkoa wa Kilimanjaro (KAA).
Nwashukuru
pia wajumbe wa Kamati Tendaji ambao walitupa ushirikiano wakiwa makao
makuu, Katibu Mkuu Msaidizi Mama Ombeni Zavalla kwa nasaha zake, Mwinga
Mwanjala na Super Star Mjumbe wa Shirikisho la Riadha Ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati, na Katibu Mkuu Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC),
Meja mstaafu Filbert Bayi, Peter Mwita (Starter wa Kimataifa), na Mjumbe
wa Kamti Tendaji, Mzee Christian Matembo kutoka Songea.
Kwa
namna ya kipekee kabisa naomba pia niwapongeze MKURUGENZI WA MASHINDANO
Ndg. Robert Kalyahe kwa kuongoza mbio kitaalamu na Mweka Hazina Gabriel
Liginyan, kwa kuhakikisha malipo yote yanakwenda sawa.
Nje
ya kamati tulikuwa na bingwa mara mbili wa Jumuiya ya Madola Mzee
Gidamis Shahanga, Alfredo Shahanga, rais mstaafu Francis John bila
kusahau wataalam waliopima njia kisomi kabisa – John Bayo, Anthony
Mwingereza na Naasi Gwage.
Kamati maalum ya Cross Country Series tunawapa pongezi kwa ubunifu mzuri.
Aidha,
pongezi za kipekee zimwendee Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida,
ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Riadha Mkoa wa Singida, Miraji Jumanne
Mtaturu, kwa ushirikiano wake mkubwa katika maendeleo ya riadha, ikiwamo
kujitolea kufanikisha mashindano ya wazi kwa mikoa ya kanda ya kati ya
vijana, ambayo yatafanyika mwezi ujao maalumu kupata timu ya Taifa ya
Vijana kwa ajili ya mashindano ya vijana ya Ukanda wa Afrika Mashariki
na Kati, ambako Tanzania itakuwa mwenyeji.
Kwa
unyenyekevu mkubwa, tunawaomba watanzania kwa ujumla kutupa sapoti kwa
ajili ajili ya maandalizi ya Timu hii ya Taifa ya Nyika, ikiwamo kambi
ambayo itaanza mara baada ya mashindano ya Mbio za Kilimanjaro Marathon
mjini Moshi.
No comments:
Post a Comment