Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akisaini kitabu cha wageni
alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mapema leo
asubuhi (kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Thobias Andengenye.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye aliyekaa katikati mbele
akiwatambulisha Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo kwa Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala na kumueleza ni jinsi gani Jeshi
la Zimamoto linavyoendesha shughuli zake.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akimkabidhi zawadi ya bendera
ndogo ya mezani Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna
Makakala ikiwa ni ishara ya umoja, ushirikiano na ukumbusho juu ya ziara
yake alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jengo la ushirika – mnazi
mmoja mapema leo asubuhi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kushoto) akiwa kwenye picha ya
pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala
(kulia) mapema leo asubuhi alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akiwa kwenye picha ya pamoja na
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala na Viongozi
Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto mapema leo asubuhi.
(PICHA NA FC GODFREY PETER)
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye atembelewa na Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala lengo ni kujifunza na kukuza
mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili vya Ulinzi na Usalama.
Katika ziara hiyo Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, alitumia
fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Uhamiaji na kumuahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Uhamiaji Dkt. Anna Makakala ametembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji yaliyopo jengo la ushirika – mnazi mmoja jijini Dar es
salaam, mapema leo asubuhi na alipata fursa ya kujifunza jinsi gani
Jeshi hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kuwa na mazungumzo ya
kina na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na
Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo. “Nimejifunza mengi lakini pia
nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza
kushirikiana” alisema Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt Anna
Makakala
No comments:
Post a Comment