Monday, 27 February 2017

Uongozi wa klabu ya Yanga, umewaomba radhi mashabiki na wanachama

Uongozi wa klabu ya Yanga, umewaomba radhi mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kwa matokeo mabaya waliyoyapata juzi Jumamosi dhidi ya Simba.
Katika mchezo huo Yanga ilifungwa bao 2-1 na Simba mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amewaomba radhi mashabiki, wanachama na wapenzi wa timu hiyo kuendelea na utulivu wao katika kipindi hiki ambacho wamepoteza mechi muhimu.
“Matokeo haya tuliyopata ni ya kimchezo, kikubwa ni kupambana na michezo iliyobaki mbele yetu na kuendelea kuwapa ushirikiano wachezaji kwani bado tuna mashindano mengi na michezo mingi mbele yetu, tunaamini kocha ameona mapungufu kwenye mchezo uliopita na atayafanyia kazi na kurejesha furaha yetu,” inasema taarifa hiyo ya Mkwasa.

Yanga wanajiandaa na mechi ya kiporo dhidi ya Ruvu Shooting itakayochezwa keshokutwa Jumatano na Machi 05, itakuwa na kibarua kingine kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar.

No comments:

Post a Comment