Antoine Griezman(Athletico Madrid).Anaweza kufikia hata thamani ya £100m kwa sasa.Ni mchezaji watatu kwa ubora duniani akiwa nyuma ya Messi na Ronaldo,Griezman ameanza kuhusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United,ameshawahi kukiri ugumu wa yeye kuhamia katika vilabu vya Hispania (Madrid na Barcelona).Lakini pesa za miamba hiyo miwili zinaweza kuvunja rekodi ya usajili aliyonayo Pogba kwa sasa.Kuwepo katika tatu bora ya Ballon D’or na mchezaji bora wa FIFA sio kitu kidogo na kinaweza kulifanya dau lake la usajili likawa kubwa kuliko la Pogba.
Neymar Jr(Barcelona).Tafiti mbali mbali zimemtaja Neymar kama mchezaji ambaye thamani yake ndani na nje ya uwanja,ni wazi kwamba Neymar hawezi kung’ara sana akicheza pembeni ya Messi,yupo katika timu ambayo nafasi ya ushambuliaji kuna wafalme wengine.Ili Neymar awe mkubwa zaidi ni lazima awe katika timu ambayo ataonekana mkubwa.Anahusishwa na kuuzwa timu mbalimbali ikwemo PSG na United hawachezi mbali.Lakini unadhani uhamisho wa Neymar utakuwa wa kitoto?laa hasha Neymar ni lazima atasajiliwa kwa rekodi itakayoishtua Dunia.
Lioneil Messi(Barcelona).Mashabiki hawana shukrani ,katika mchezo wa Barcelona dhidi ya PSG kulikuwa na kikundi kidogo cha mashabiki waliokuwa wakimzomea Messi.Kitendo hiki kilimkera Muargentina huyu mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara 5.Mechi iliyofuata ya Barcelona hakushangalia baada ya kuifunga Leganes.Haina maana kubwa kwamba itamfanya Messi aondoke Barcelona lakini kuna uwezekano mkubwa hilo likatokea siku moja.Matajiri wa Chelea na Man City tayari wameangalia pochi zao kuhusu hilo na lazima watapaswa kuchomoa kiasi kikubwa sana cha pesa katika akaunti zao ili kupata sahihi ya Messi.
Pierre Aubemayang(Borussia Dortmund).Dortmund kila mwaka wamekuwa wakiuza mchezaji mkubwa,Lewandoski,Gotze,Kagawa,Hummels ni mfano wa hili.Tayari Aubemayang ameshaeleza ndoto yake ya kucheza Madrid siku moja.Naamini raisi wa Madrid Florentino Perez ameliona hili,wakati ni huu Cr7 umri unamuacha na ameanza kupungukiwa na njaa ya magolu,Benzema nae haeleweki huku akiwa na matukio mengi nje ya uwanja.Lazima Madrid watafute mtu wa kuziba pengo la Cr7.Umri wa Aubemayang ni mdogo na kiwango chake kinaeleweka jinsi kilivyo kikubwa hii inaweza ikamfanya Perez asione tabu kuvunja rekodi ya usajili ya Pogba kwa Mgabon huyu.
Paulo Dyabala(Juventus).Tayari ameanza kutajwa kama Lioneil Messi mpya.Miaka 23 na uwezo ulioko miguuni mwake unatia mashaka kuhusu Dyabala kubaki Juventus kwa muda mrefu.Jina lake ni kati ya majina ambayo yapo sana katika tetesi za usajili.Timu nyingi kubwa ikiwemk Chelsea,Real Madrid,Bayern Munich na Paris Saint German zimekuwa zikifuatilia kwa karibu maendeleo ya Dyabala,hii inamfanya Dyabala thamani yake kuonekana kubwa sana kutokana kugombewa na timu kubwa.
Delle Alli(Totenham Hotspur).Kama ilivyo kwa Dyabala,Alli ni kinda mwingine anayezungumziwa sana kwa sasa.Tetesi zinasema Barcelona walikaribia kumnunua Alli katika dirisha la usajili lililopita kabla ya kushindwana dau na Totenham.Lakini kadri siku zinavyoenda Alli anaonekana kuzidi kuimarika na kuzivutia timu nyingi zaidi na hii pia haitashangaza akisajiliwa usajili wake ukawa wa gharama kubwa.
No comments:
Post a Comment