Timu ya taifa ya Cameroon itakutana na Misri katika fainali ya Kombe la
Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Ghana usiku wa jana
katika Nusu Fainali ya pili Uwanja wa Franceville mjini Franceville,
Gabon.
Simba Wasiofungika walistahili ushindi huo kutokana na kutawala mchezo kuanzia mapema na kuwapoteza kabisa Black Stars.
Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, Ngadeu-Ngadjui akifungia bao la kwanza Cameroon dakika ya 72 kabla ya Bassogog kufunga la pili dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo.
Cameroon
Kikosi cha Cameroon kilikuwa: Ondoa, Fai, Ngadeu-Ngadjui, Teikeu, Oyongo
- Siani, Djoum/Mandjeck dakika 77, Zoua - Moukandjo, Ndip
Tambe/Aboubakar dk73 na Bassogog.
Ghana: Razak, Acheampong, Boye, Amartey, Afful - Wakaso, Acquah/Gyan dk76, Partey/Agyemang-Badu dk86, Atsu, A.Ayew na J.Ayew.
No comments:
Post a Comment