Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano (NIDA) Bi. Rose Mdami, akimkabidhi Kitambulisho chake Mhe.
Mashimba Mashauri Ndaki, Mbunge wa Maswa Magharibi alipofika kuchukua
kitambulisho chake leo Dodoma.
Mhe. Peter Msigwa Mbunge wa
Iringa Mjini, akikabidhiwa Kitambulisho chake leo bungeni na Afisa
Usajili mkoa wa Dodoma Ndg. Khalid Mrisho.
Mhe. Leonidas Gama, Mbunge wa Songea mjini, akisaini kitabu kuthibitisha kukabidhiwa Kitambulisho chake cha Taifa leo Dodoma.
Akikagua orodha yenye majina ni
Mh. Yahaya Omary Massare Mbunge wa Manyoni Magharibi, wakati alipofika
kuchukua kitambulisho chake cha Taifa Bungeni Dodoma leo. Kulia ni Ndg.
Khalid Mrisho Afisa Usajili mkoa wa Dodoma.
Mh. Mariam Nassoro Kisangi
(Mwenye kilemba kulia), Mbunge wa Viti Maalumu akipata maelezo ya
kitambulisho chake kipya toka kwa Bi. Rose Mdami Kaimu Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano NIDA.
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA) imeanza zoezi la Ugawaji Vitambulisho vya Taifa vipya kwa
waheshimiwa Wabunge wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wanaondelea na kikao chao mjini Dodoma.
Pamoja na kugawa Vitambulisho,
NIDA inaendelea kuwasajili waheshimiwa Wabunge ambao hawakusajiliwa
awali. Lengo ni kuhakikisha Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania wana Vitambulisho vya Taifa na kuvitumia kwenye shughuli
mbalimbali za utambuzi hususani kwenye Taasisi na makampuni binafsi
yenye kutoa huduma kulingana na teknolojia itakavyoruhusu.
No comments:
Post a Comment