Ishu
kubwa sasa hivi Dar es salaam ni dawa za kulevya ambapo leo February 6
2017 Kamishna wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro
amezungumza na Waandishi wa habari na kutoa takwimu ya kilichofanyika
ndani ya siku 3.
“Tunaendelea vizuri na Oparesheni yatu ya kupambana na dawa za kulevya,
tumekamata jumla ya Watuhumiwa 112 na jumla kete 299 zidhaniwazo kuwa ni
dawa za kulevya, kwa kawaida tutazipeleka kwa mkemia mkuu wa Serikali
na atatuambia ni aina gani”
“Katika Watuhumiwa hao 112, 12 tumewapeleka leo Mahakamani sababu sheria
ya mwenendo wa mashtaka iko wazi, huwa inaturuhusu kuomba kuwaombea
Watuhumiwa kwa kiapo kwa Hakimu, wawe chini ya uangaliazi wa Jeshi la
polisi na Mahakama kwa muda wa miaka miwili wasifanye makosa tena‘
“Wote tuliowakamata wengine wanakiri na wamekwenda kuonyesha hizo dawa
za kulevya, kusudio la kwanza ni wawe chini ya uangalizi wetu na kusudio
la pili la kiapo chetu ni waache hiyo tabia wawe raia wema, kusudio la
tatu wawe wanakuja kuripoti kituo cha polisi angalau mara mbili kwa
mwezi…. lengo letu ni kuona je wameacha kutumia dawa za kulevya?” –
Kamishna Simon Sirro
No comments:
Post a Comment