Maafisa watatu wakuu wa kijeshi ndani ya serikali ya Sudan Kusini, wamejiuzulu.
Makamanda hao wamejiondoa serikalini wakimlaumu Rais Salva Kiir kwa
kuhusioka katika uhalifu wa kivita na mauwaji yanayolenga kabila fulani.
Brigedia Henry Oyay Nyago, anamshutumu Rais, ambaye anatoka katika
kabila la Dinka, kwa kuamuru kuwawa kwa watu wasiotoka katika kabila
hilo la Dinka.
Kanali Khalid Ono Loki, pia anamlaumu kiongozi mkuu wa jeshi kwa mauwaji ya kimbari, kukamatwa na kuwazuilia watu kiholela.
No comments:
Post a Comment