Friday, 2 September 2016

William Ole Ntimama amefariki Dunia siku wa kumkia leo

 
Kenya inaomboleza kifo cha mwanasiasa mkongwe William Ole Ntimama aliyefariki usiku wa kumkia leo akiwa na mri wa miaka 86.
Hadi kifo chake, Bwana Ole Ntimama alikuwa kiongozi wa shupavu wa jamii ya Wamaasai. Hivi majuzi, Ntimama alikihama chama cha upinzani, ODM, na kujiunga na muungano wa Jubilee unaotawala Kenya. Ntimama alihudumu katika serikali ya Hayati Mzee Jomo Kenyatta akiwa mwenyekiti wa Kauti ya Narok iliyo eneo la mbuga maarufu ya wanyamapori ya Maasai Mara na pia kama waziri katika wizara mbali mbali wakati wa utawala wa Rais Msaafu Daniel arap Moi na Rais Mwai Kibaki. Risala za rambirambi zinaendelea kumiminika kutoka kwa viongozi mbalimbali wakimtaja mwanasiasa huyo kuwa mtetezi wa haki za jamii za wachache. Kwenye risala yake, Rais Uhuru Kenyatta amemtaja Marehemu Ole Ntimama kama kiongozi aliyejitolea kuhudumia taifa katika miaka yake yote ya kisiasa.

No comments:

Post a Comment