Ofisi ya gazeti la Tanzania Daima yatolewa vitu nje kutokana na deni
Madalali wa NHC wamefika katika ofisi za gazeti la Tanzania
Daima asubuhi hii na kuanza kutoa vifaa ofisini kutokana na deni la
pango la mmiliki wa gazeti hilo, Freeman Mbowe.
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Neville Meena amesema wako kwenye
msukusuko mkubwa lakini wanafanya jitihada za kukabiliana na hali hiyo
ili kuhakikisha uzalishaji wa gazeti unafanyika kama kawaida.
No comments:
Post a Comment