Mke wa mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donal Trump, Melania Trump amelishtaki gazeti la Daily Mail la Uingereza pamoja na mwanablogu wa Marekani akitaka alipwe $150m (£114m) sawa na Tsh trilioni 326 kuhusiana na tuhuma kwamba alikuwa kahaba miaka ya 1990, wakili wake amesema.
Gazeti la Daily Mail lilidokeza kwamba huenda Trump alifanya kazi ya muda kama kahaba New York, na kwamba alikutana na mumewe Donald Trump, ambaye kwa sasa anawania urais, mapema kuliko inavyodaiwa.
Donal Trump akiwa na mke wake Melania Trump.
Madai hayo ni “uongo mtupu, wakili wake Charles Harder amesema.
“Washtakiwa walitoa tuhuma kadha kuhusu Bi Trump ambazo ni za uongo 100% na kumharibia sana sifa,” Bw Harder alisema kupitia taarifa.
Bi Trump, 46, alizaliwa Slovenia na akahamia Marekani kufanya kazi kama mwanamitindo miaka ya 1990.
Aliolewa na Bw Trump mwaka 2005.
No comments:
Post a Comment