Gari lilivyowaka.
Mashuhuda
Mashuhuda.
MOROGORO: Dereva wa gari dogo la mizigo aina ya lsuzu Carry (Kirikuu) lenye namba za usajiri T 609 CKW, amenusurika kifo baada ya gari hilo alilokuwa akiendesha kuwaka moto katika eneo la Masika katikati ya Mji wa Morogoro, leo
Wakizungumza na mwanahabari wetu aliyefika eneo la tukio, mashuhuda wa tukio hilo Bernard Joseph na Juma ldd walisema;
“Huyu dereva wa kirikuu alikuwa akitokea eneo la Msamvu (Kituo Kikuu cha Mabasi Yaendayo Mikoani) alipofika hapa Maska jirani na ‘round about’ tulishuhuida gari lake likiwaka moto kwa nyumba na yeye hakuwa na habari aliendelea na safari hivyo boda boda mmoja aliamua kuwasha pikipiki yake na kumkimbilia na kumjulisha tukio hilo ambapo alisimama na kushuhudia gari hilo likiendele kuwaka moto,” walisema mashuhuda hao
Kwa upande wake dereva wa gari hilo aliyejitambulisha kwa jina la Michael Augustino alisema.
“Nashangaa sana huu moto ulikotokea, gari hili injini iko mbele iweje moto utokee huku nyuma ambako hakuna kitu chochote na kama unavyoona sikuwa na mzigo wowote ndani ya gari na washukuru hawa boda boda wa hapa Masika wamenikimbilia na kunipa taarifa za moto huo, vinginevyo ungefika huku mbele kiwa kwenye mwendo wa kasi nahisi milango ingeji-lock na mimi ningeuungua vibaya,”
“Namshukuru Mungu kwa hili”alisema Agostino huku akipiga simu kwa mmiliki wa gari hilo.” Alisema Michael.
Askali wa Kikosi Maalum cha Zima moto, mwenye cheo cha nyota Moja akimhoji dereva wa gari hilo huku wakikagua kifaa Maarumu cha kuzima moto kilichokuwa ndani ya gari hilo.
No comments:
Post a Comment