Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika ya Shirika la Fedha Duniani, IMF Abebe Selassie.
Kushuka kwa bei ya mafuta katika miaka miwili iliyopita kumetikisa uchumi wa nchi nane Afrika.
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika ya shirika la fedha duniani IMF
Abebe Selassie, ametaja nchi zilizoathirika zaidi kuwa ni pamoja na
Angola, Equatorial Guinea na Nigeria ambazo zimeshuhudia kushuka kwa bei
ya mafuta kutoka dola 125 kwa pipa hadi dola 50.Athari ni pamoja na kupungua kwa kasi ya mapato ya kuuza bidhaa nje na nakisi ya fedha.
Hata hivyo kushuka kwa bei ya mafuta kumekuwa na faida kwa nchi ambazo zinatarajia kuzalisha mafuta kama Tanzania na Msumbiji kwa kuwa nchi hizo hazijaanza kuzalisha mafuta hivyo hawataathiriki na kushuka kwa bei.
Aidha ametoa wito kwa watunga sera katika nchi hizo kuzingantia uchumi mseto kama uzalishaji wa nishati, ukuzaji wa sekta ya kilimo ili kuepuka na kutegemea mapato ya mafuta pekee.
No comments:
Post a Comment