Vyombo vya Habari nchini
Vimetakiwa kuzingatia weledi katika kutimiza majukumu yake ili kusaidia
Taifa kufikia maendelo ya kweli na endelevu.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini
Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa
mkutano na vyombo vya habari.
Akifafanua Mhe. Mwakyembe
amesema ili Taifa liwe na Maendeleo ni lazima kuwa na Vyombo vya Habari
vinavyozingatia weledi wa taaluma ya uandishi wa habari pamoja na Sheria
na Kanuni zinazosimamia tasnia hiyo.
“Navipongeza Vyombo vingi vya
Habari hapa nchini ambavyo vinafanya kazi nzuri ya kuelemisha Umma na
kuchochea maendeleo ya nchi yetu ila kuna wachache ambao kwa makusudi
wameamua kupotosha Umma” alisisistiza Dkt. Mwakyembe
Hivi Karibuni gazeti moja lilitoa
taarifa zinapotosha Umma kwa kumhusisha Waziri huyo na maswala ya
Ufisadi ambapo alitumia fursa hiyo kuviasa vyombo vya habari kuepuka
kuandika au kusambaza habari ambazo ni za upotoshaji na hazina maslahi
kwa Taifa na hazijafanyiwa uchunguzi wa kina.
Akitolea mfano chombo hicho cha
habari Mwakyembe amesema kuwa, kimekuwa kikiripoti taarifa zinazogusa
masuaa ya Ulinzi na Usalama pasipo kuangalia maslahi ya Taifa kwanza
hali inayoonyesha kukosekana kwa uzalendo.
Mwakyembe aliongeza kuwa tasnia
ya habari imekuwa na ni vema sasa waandishi wote kuzingatia maadili ya
taaluma hiyo ili kuepuka kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa
kukiuka sheria na kanuni za uandishi wa habari.
Tasnia ya Habari ni muhimili
muhimu katika kuchochea Maendelo ya Taifa lolote lile kwa kuelimisha
kuhamasisha na kuamsha ari ya wananchi kujiletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment