Wednesday, 22 June 2016
Umuhimu wa Parachichi katika mwili wa binadamu
Na Kalonga Kasati
Vitu vya asili navyo vinasaidia kuweka ngozi kuwa nzuri wakati wowote ule, ngozi ni kiungo kikubwa kwa binadamu hivyo inatakiwa kuwa waangalifu kuitunza ili kuepusha isizurike na kitu kingine chochote.
Ngozi ni kiungo ambacho kinachopokea magojwa haraka hivyo ndio maana tunaambiwa ni vizuri kuitunza ili isipoteza uasilia wake.
Ngozi nzuri ni ile ambayo haijapoteza uasilia wake wakati wote na kila siku uonekana vilevile ilivyo lakini hiyo inatokana na jinsi mtu anavyoweza kuitunza ngozi hiyo.
Kwa upande wa wanawake tunathamini mno ngozi ya usoni tofauti na sehemu nyingine katika mwili, kwani ngozi ya uso ni muhimu na vilevile ni rahisi kushika vigonjwa vidogovidogo ambavyo vinavyokuwa vinaharibu ngozi yako.
Hakuna mwanamke asiyependa ngozi ya sura yake haijarishi kama sura yake ni mbaya au nzuri lakini ilimradi tu ngozi yake iwe nzuri na safi.
Wanawake hutumia pesa nyingi kwa ajili ya kununua vipodozi vya usoni ili kuweka ngozi yake kuwa nzuri wakati wowote ule.
Lakini vipodozi vingi ambavyo vinavyotumiwa na wanawake vina sumu ya kemikali ambayo wakati mwingine inasababisha kuharibu ngozi ya mtumiaji wa hicho kipodozi.
Ndio maana wataalam wa masuala ya ngozi wanashauri wanawake kuwa makini katika uchaguzi wa vipodozi wanavyotumia ili wasiweze kudhurika.
Ngoja nirudi katika mada yetu ambayo tuliyokusudia leo ya kutumia vitu mbalimbali ambavyo vitakavyowezesha kuwa mrembo zaidi na ngozi kuwa nzuri wakati wote ule.
Matunda kama parachichi, tango limao, matunda haya mara nyingi ukitumia usoni inakufanya ngozi yako kuwa nzuri na nyororo wakati wowote ule.
Uzuri wa matunda haya hayana kusema kuwa umekosea masharti au umezidisha dozi matunda haya hata ukipaka kwa wingi usoni kwako haviwezi kuleta athari yeyote katika ngozi yako.
Pia mafuta ya mawese nayo nayasaidia kuifanya ngozi yako kuwa laini na kung'aa na vilevile inasaidia kuondoa taka zote zilizokuwa usoni.
Hata unga wa dengu nao unasaidia kupendezesha sura yako hasa ukichanganya na kiini cha yai ya kuku wa kienyeji.
Mafuta ya nazi nayo yanasaidia kuondoa harara usoni na kuifanya sura yako ipendeze wakati wote, hivyo vitu kama hivi mara nyingi vinasaidia kutoondoa uasili wa rangi ya ngozi yako siku zote.
Wapo wanawake wanaotumia vitu vaya asili na ukiwaona sura zao huwa ni nzuri wakati wote na wanakuwa hawabadili uasili wa ngozi yao .
Kama ni mweupe utakuwa ni mweupe vilevile ila atakuwa anaufanya weupe wake uwe na thamani kwani wakati wote atakuwa anang'ara na kupendeza.
Na kama mweusi atabaki na rangi yake hiyo hiyo ila itakuwa ni mweusi wa kupenda na kila wakati utakuwa unamtamani kwa sababu ya rangi yake ya asili.
Urembo wa asili uanaweza kutumiwa hata na watoto waliochini ya miaka 18 kwa kuwa haudhuru ngozi na kutosabisha magojwa ya ngozi.
Vipodozi vyenye kemikali mara nyingi husababisha kupotea kwa rangi yako asilia na vilevile husababisha ugojwa wa saratani ya ngozi ambayo mwisho wake husababisha kifo.
Labels:
MWANZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment