Kesi ya madai iliofunguliwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuiomba mahakama kupiga marufuku zuio la Polisi, leo limetupiliwa mbali.
Mbowe
alifungua kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, baada ya hivi karibuni
Jeshi la Polisi kupiga marufuku mikutano ya hadhara kwa madai kwamba,
hali ya usalama nchini si salama.
Mbowe
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro katika shauri hilo,
aliwashtaki Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali (AG), kwa madai wanahusika kuzuia kufanyika kwa mikutano ya
hadhara ya vyama vya siasa.
Mbowe
ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, walitangaza kufanya
oparesheni iliyopewa jina ‘Okoa Demokrasia nchini’ iliyokuwa na lengo la
kuishtaki serikali kwa wananchi kwa kile alichodai, kuendesha nchi bila
kufuata katiba ya nchi.
Hata
hivyo, baada ya kupigwa marufuku kwa maandamano, Mbowe alifungua kesi
ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, akiiomba
kutengua zuio hilo la polisi.
Mohammed
Gwae, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, leo amepitia
ombi lililopelekwa mahakamani hapo na upande wa mlalamikaji
anayewakilishwa na mawakili John Mallya na Gasper Mwanalelya na kutoa
uamzi.
Jaji
Gwae akitoa uamuzi wa ombi la walalamikaji amedai kuwa, amefikia hatua
hiyo baada ya walalamikaji kukosea kifungu cha kupeleka shauri hilo
kortini kitendo kilichosababisha kulitupilia mbali.
Amesema
kuwa, walalamikaji baada ya kupeleka ombi hilo kortini, upande wa
wajibu maombi unaoongozwa na mawakili, Seth Mkemwa na Robert Kidando
waliweka pingamizi wakiomba mahakama kutokusikiliza ombi hilo.
Jaji
Gwae amesema kuwa, walalamikaji katika ombi lao walikosea kutumia
kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu cha sheria ya mwaka 2014 badala
ya kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili ambacho kilitakiwa kutumiwa.
“Waleta
maombi wametumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu badala ya
kutumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili kilichotakiwa kuwepo
katika kuleta ombi na kama kifungu hiki hakijatumika hapo na ombi
halipaswi kupokelewa,” amesema Jaji Gwae.
Hata
hivyo Jaji Gwae amesema, licha ya kuwekewa pingamizi na wajibu maombi,
walalamikaji wamesema kanuni na kifungu hicho ndivyo vilitakiwa kuwepo
na hivyo vinavyopaswa kuwekwa sio sahihi.
Amesema
kuwa, katika shauri la namna hiyo, kanuni na vifungu vilivyotakiwa
kuwepo ni kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili na kanuni ya tano na
kifungu kidogo cha sheria ya mwaka 2014 na kwamba wao waliviweka katika
maelezo (Statements) badala ya (chember samers).
Mallya,
mwanasheria wa mpeleka maombi amesema kuwa, baada ya kukosea kanuni na
vifungu hivyo, watapeleka kwa mara nyingine ombi na kulifanyia
marekebisho kama Jaji Mohamed Gwae alivyoelekeza.
No comments:
Post a Comment