Wednesday, 1 June 2016

Kesi ya Kizza Besigye yaahirishwa tena

Kesi ya Kizza Besigye yaahirishwa tena
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Dk.Kizza Besigye aliyekuwa anatarajiwa kufikishwa Mahakamani leo kujibu shtaka la uhaini hajafikishwa mahakamani.
Upande wa mashtaka umeomba ruhusa mahakama hiyo ihamishwe karibu na gereza alikozuiliwa Bw Besigye kwa ajili ya tishio la amani mjini.


Hata hivyo viongozi wengine wa upinzani wamejaa mahakamani ambapo wanafanya mgomo baridi.
  • Besigye ashtakiwa kosa la uhaini Uganda
  • Besigye ahamishiwa gereza la Kampala
  • B esigye akamatwa kwa 'kujiapisha' Uganda
Hakimu aliyekuwa anatarajiwa kusikiza kesi hiyo aliagiza kuahirishwa kwa kusikizwa kwa kesi hiyo hadi tarehe 15 mwezi huu wa sita.

Bw Besigye ndiye aliyekuwa mshindani wa karibu wa Yoweri Museveni katika uchaguzi mkuu wa February 2016.
Kiongozi huyo wa upinzani anadai kuwa alishinda katika uchaguzi huo, ambao ulikosolewa na wangalizi wa kimataifa.


Bw Besigye ndiye aliyekuwa mshindani wa karibu wa Yoweri Museveni katika uchaguzi mkuu wa February 2016.
Hatua yake ya kujiapisha kuwa rais ndiyo iliyomkasirisha rais Museveni ambaye ndiye ameanza hatamu yake ya tano uongozini na kusababishwa kukamatwa kwake kwa kukiuka katiba kwa kosa la uhaini.

Besigye amekuwa akishikiliwa na polisi kwa muda wa siku kumi na mbili baada ya mahakama huko Moroto kuagiza awekwe rumande hadi Juni mosi.

Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wafuasi wake ambao wamekuwa wakisema hakuruhusiwa kuwasiliana na wanasheria wake.

No comments:

Post a Comment