Hillary Clinton amesogea na kupungukiwa na kura 20 tu kuweza kupata uteuzi wa chama chake cha Democratic, baada ya ushindi katika eneo la Marekani katika visiwa vya Karibia la Puerto Rico
Ushindi huo pamoja na ushindi wa Jumamosi katika visiwa vya Marekani vya Virgin unamfanya Clinton kubakia na upungufu wa wajumbe maalum 20 kati ya wajumbe 2,383 anaohitaji kupata kuteuliwa na ushindi huo unampa msukumo kuelekea katika jimbo la mwisho kesho.
Wakati karibu asilimia 70 ya kura zimekwisha hesabiwa, Clinton alikuwa anaongoza kwa asilimia 59.38 ya kura, akimtangulia Bernie sanders ambaye amepata asilimia 37.53.
Puerto Rico ina wajumbe maalum 67, wengi wao watagawanywa kati ya wagombea kwa misingi ya matokeo ya uchaguzi huo wa jana.
No comments:
Post a Comment