Meneja
Mahusiano Mwandamizi wa Benki ya Posta Tanzania Noves Moses(katikati)
akionyesha fedha kissing cha shilingi milioni 8 zilizotolewa na Benki
hiyo kwa ajili ya kuwasaidia vijana waendesha bodaboda wa Wilaya ya
Biharamulo. Wa kwanza kushoto Ni Mbunge wa jimbo la biharamulo Oscar
Mukasa, Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Darry Rwegasira na kulia Ni Diwani
wa kata ya Biharamulo mjini David Mwenenkundwa na Meneja wa TPB tawi la
Bukoba Juvestina Tarimo.
Na Angela Sebastian, Biharamulo.
WAENDESHA pikipiki zinazofanya biashara ya kubeba abiria
katika Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wameshauriwa kujiunga katika
vikundi rasmi na vya uzalishaji mali ili waweze kunufaika na fursa za
huduma za kibanki ambazo hutolewa na banki ya posta Tanzania.
Ushauri
huo ilitolewa jana na mkuu wa Wilaya hiyo Darry Rwegasila wakati
akifungua mafunzo ya waendesha pikipiki zaidi ya 100 waliopata mafunzo
ya udereva na kupewa leseni kwa udhamini wa banki ya posta hiyo.
Rwegasila alsema kuwa umoja ni nguvu kwahiyo wakiunda umoja wanakuwa na sauti moja pia hata viongozi wataweza
kupata mawazo yao kwa urahisi kupiti umoja huo ili kuwatafutia fursa
mbambali au kutatua changamoto zao zinazowakabili na kupandisha uchumi
wao wa kipatao.
Alisema
kuwa makondi hayo yatasaidia kuingia katika mfumo rasmi ambao
utawawezesha kupata huduma zinazotolewa na taasisi mbalimbali kama vile
banki ya posta ambazo zinalenga kuwakwamua vijana katika lindi la
uamskini unaowakabili pia unaonekana kuwa kero kubwa katika maisha yao ya kila siku.
“Mkitaka
kuingia katika soko hulia lazima muwe na umoja ili muweze kufikia
raslimalia zinazopatikana kama vile kupata misaada,mikopo na mafunzo
kama haya waliowaletea watu wa banki ya posta kutokan ana faida
wanayoipata na kugawana na wahitaji” alisema Dc.
Pia
aliwashauri kuacha kufanya matumizi yasiyo ya maana ,bali watumie
kidogo wanachokipata kujiwekea akiba banki ili waweze kukuza mitaji yao
kwani wao ni vijana bado wanamahitaji mengi.
Kwa
upande wa meneja mahusiano mwandamizi wa banki ya posta Tanzania Noves
Moses alisema kuwa banki hiyo inajali wananchi ,pia vijana ni kundi
kubwa lenye mchango mkubwa katika suala zima la uchangiaji wa uchumi wa
Taifa.
Alisema
banki hiyo walipata maombi toka kwa mbunge wa jimbo la Biharamulo
Oscara Mukasa akiomba kuwawezesha vijana hao kupata mafunzo na kupewa
leseni ili kuondoka ana adha ya kukimbizana na polisi kila kukicha na
kupoteza muda mwisngi ambapo hushindwa kujiingizia kipatao.
Alisema
banki hiyo ilikubali ombi hilo ambapo ametoa kiasi cha shilingi milioni
8 kwa ajili ya mafunzo hayo ya kupata leseniya uendeshaji wa vyombo
hivyo vya moto kwa vijana 100 kwa Wilaya ya hiyo.
Alisema
kuwa banki hiyo imejiwekea mikakati mikubwa ya kuleta na kuimalisha
ustawi wa ndani ya jamii ambapo misaada mingi wanayoitoa huelekezwa
katika eneo hilo ambayo hulenga masuala ya afya na elimu.
Naye
mbunge wa jimbo la Biharamulo aliyeomba msada huo kwa ajili ya vijana
wake Oscar Mukasa alisema kuwa ni wajibu wake kuboresha maisha ya vijana
waliko jimboni mwake ili waondokane na mambo yanayoweza kuwapelekea
kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo uvunjifu wa amani na maandamano
yasiyofaa.
Mukasa
alisema lengo la kuomba banki hiyo itoe msaada huo ni kuhakikisha vijana
wanaepukana na maisha ya misukosuko ya kukosa leseni ambayo walikuwa
wakikumba na nayo.
No comments:
Post a Comment