Kaimu
Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad Kawawa (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam mchana
huu wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma zilizotolewa na mwandishi wa ”
The Ecomist” Gazeti la Kiingereza linatoka kwa wiki dhidi ya Serikali
ya Tanzania. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TCI), Daud Biganda.
Meneja
Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TCI), Daud Biganda (kulia),
akitoa ufafanuzi wa Uchumi tangu Rais Dk. John Magufuli aingie madaraka
na miradi iliyosajiliwa na kituo hicho.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Taarifa akichukuliwa na wanahabari.
……………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI
imekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Kiingereza linalopaka kila
wiki lililodai kuwa Rais Dk.John Magufuli anaongoza nchi kwa msukumo
licha ya kuonekana mzuri na kuwa taarifa hiyo imelenga kuupotosha umma.
Habari
iliyoandikwa kwenye gazeti hilo ilikuwa na kichwa kilicho andikwa
“Government by gesture, A President who looks good but governs
impulsively”
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa ufafanuzi
wa habari hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad
Kawawa alisema taarifa hiyo haikuwa na uzalendo na amewataka wanahabari
kuwa makini na habari zenye mlengo wa kupotosha taifa.
“Nawaombeni wanahabari wenzangu kuweni makini na taarifa zenye mlengo wa kupotosha umma” alisema Zamarad.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu suala la uchumi Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC), Daud Biganda alisema taarifa hiyo siyo sahihi na
imelenga kupotosha na inavuruga ukweli kwani Tangu Rais Dk.John Magufuli
aingie madarakani kwa kipindi cha kati ya mwezi Desemba 2015 na 2016,
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeweza kuandikisha miradi ya
uwekezaji ipatayo 551 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni
9,211.88 kati ya miradi hiyo miradi 229 yenye asilimia 42 inamilikiwa na
watanzania, miradi 215 yenye asilimia 39 inamilikiwa na wageni na
miradi 107 yenye asilimia 19 inamilikiwa kwa njia ya ubia kati ya
watanzania na wageni.
Biganda
alisema kuwa miradi yote hiyo ya uwekezaji ilitarajiwa kuzalisha ajira
zipatazo 55,970 na kuleta matokeo mengine kwa watanzania na kuwa
imesajiliwa na TIC.
No comments:
Post a Comment