Simba SC inaendelea na kambi yake visiwani Zanzibar ikijiandaa na mchezo
dhidi ya mahasimu, Yanga Februari 25 ya Jumamosi wiki ijayo.
Nahodha wa Simba, Jonas Gerald Mkude amesema kwamba hadi sasa wako vizuri kuelekea mchezo huo wa Februari 25.
“Yanga ni timu kama timu nyingine, wao wanajiandaa na sisi tunajiandaa
na wachezaji wote wako vizuri na dakika 90 ndizo zitakazoongea,”
amesema.
Simba imekwenda kambini Zanzibar siku moja baada ya kutinga Robo Fainali
ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufuatia kuifunga 1-0
African Lyonjuzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bao pekee la Laudit
Mavugo.
Kikosi cha Simba kilichoingia kambini hapo jana kinaundwa na Makipa; Daniel Agyei, Peter Manyika na Dennis Richard.
Mabeki: Janvier Bokungu, Hamad Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi
Banda, Vincent Costa, Novaty Lufunga na Method Mwanjali.
Viungo: Jonas Mkude, James Kotei, Said Ndemla, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim,
Muzamil Yassin, Mwinyi Kazimoto, Shiza Kichuya na Jamal Mnyate.
Washambuliaji: Laudit Mavugo, Pastory Athanas, Ibrahim Ajibu, Hijja Ugando na Juma Luizio.
No comments:
Post a Comment