Sunday, 19 February 2017

Mchungaji Cosmas Mhina amewasihi vijana kutoingia katika migogoro ya kanisa



Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Kibaha mkoani Pwani, Cosmas Mhina amewasihi vijana ndani ya kanisa hilo kutojiingiza kwenye migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza katika maeneo mbalimbali ndani ya kanisa hilo na badala yake wajikite katika kutangaza amani.

Kauli ya kiongozi huyo  imekuja huku kukiwa na hali ya sintofahamu ndani ya kanisa hilo hususani Dayosisi ya Dar es Salaam ambapo hivi karibuni Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana, Dk Jacob Chimeledya alimtaka Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa kujiuzulu  wadhifa wake kwa madai kwamba anatumia vibaya madaraka yake.
Mchungaji huyo akizungumza leo kabla ya kufanyika uchaguzi wa viongozi wa vijana ngazi ya Achidikonary ya Kibaha  (TAYO) Tanzania Anglikan  Youth  Organaization uliofanyika Kibaha mkoani Pwani alisema kuwa kwa mujibu wa tetesi zilizopo ni kuwa kwa sasa wapo baadhi ya watu wameendelea kupandikaza mgogoro huo kwa njia mbalimabli.

No comments:

Post a Comment