Mamlaka nchini Afrika Kusini imewapeleka maafisa wa polisi katika baadhi ya vyuo vikuu ili kusaidia maandamano ya wanafunzi wakati wa ufunguzi wa vyuo hivyo.
Maelfu ya wanafunzi waliandamana mwezi Oktoba ili kupinga hatua ya serikali ya kuongeza karo kwa mwaka.
Wanafunzi hao wametaka kupewa elimu ya bila malipo.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema kuwa viongozi kadhaa wa wanafunzi waliokamatwa wakati wa maandamano hayo bado wanakabiliwa na mashtaka.
No comments:
Post a Comment