Rais wa Marekani Donald Trump anajiandaa kuwafanyia mahojiano wale
wanaotarajiwa kuchukua wadhifa wa mshauri wa masuala ya usalama wa
Marekani, kufuatia kujiuzulu kwa Michael Flynn.
Wale ambao wanatarajiwa kuhojiwa ni pamoja na balozi wa zamani wa
Marekani kwenye Umoja wa Mataifa John Bolton na aliye sasa kaimu mshauri
Keith Kellogg.
Majemedari wengine wawili ni H.R McMaster na Robert Caslen, pia wamo katika orodha hiyo.
Michael Flynn alijiuzulu Jumatatu ya juma lililopita, kutokana na utata
kuhusiana na vikwazo vya Marekani kwa Moscow uliomzingira baada ya
kukutana na balozi wa Urusi jijini Washington.
No comments:
Post a Comment