Friday, 30 September 2016
Nape amewatoa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa tiketi kuelekea mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara kati ya watani wa Jadi Yanga na Simba
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa
habari(hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya
matumizi ya tiketi za kieletroniki kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania
Bara ya watani wa Jadi Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi
leo ,2016.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisisitiza jambo kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya
upatikanaji wa tiketi za kieletroniki kuelekea mechi ya Ligi kuu
Tanzania Bara ya watani wa Jadi Yanga na Simba itakayochezwa kesho
Oktoba Mosi leo ,2016 kushoto ni Meneja Mradi kutoka kampuni ya Selcom
Tanzania Bw. Gallius Runyeta.
Waziri wa Habari Utamaduni sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akieleza waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya matumizi ya tiketi
za kieletroniki kuelekea mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara ya watani wa
Jadi Yanga na Simba itakayochezwa kesho Oktoba Mosi leo ,2016 kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw. Alex
Nkenyenge.
Waandishi wa Habari wakifatilia mkutano huo.
Waandishi wa Habari wakifatilia mkutano huo.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
Na Raymond Mushumbusi WHUSM
Mashabiki wa soka nchini
wameondolewa wasiwasi kuhusu upatikanaji wa tiketi kuelekea mchezo wa
ligi Kuu Tanzania Bara kati ya watani wa Jadi Yanga na Simba na
kuhakikishiwa kuwa mfumo wa upatikanaji tiketi uko vizuri na mpaka sasa
tiketi zinaendelea kuuzwa katika maeneo mbalimbali.
Wasiwasi huo umetolewa na Waziri
wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu
matumizi ya tiketi za kieletroniki kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania
Bara kati ya Yanga na Simba.
Waziri Nape amesema kuwa kuna
kuna taarifa kutoka mitaani kuwa kuna uwezekano wa mfumo huu kutofanya
kazi katika mechi hii na malalamiko ya watu wengi kulalamika kukosa
tiketi za mchezo wa kesho.
Tunda Man na Jaguar wa Kenya wafanya kolabo
Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Tunda Man amesema kolabo ambayo inakuja kutoka kwake ni ile aliyofanya na msanii wa Kenya, Jaguar.
Muimbaji huyo ameiambia FOFAM-MEDIA BLOG kuwa ana kolabo nyingi ambazo amefanya na wasanii mbalimbali lakini kolabo ambayo amepanga kuitoa hivi karibini ni ile aliyofanya na Jaguar.
“Kuna kolabo nyingi ambazo nimefanya na wasanii wa hapa pamoja na nje lakini kolabo ambayo mpaka sasa ipo kwenye mpango wa kutoka ni kolabo ambayo nimefanya na Jaguar, kwa hiyo mashabiki watulie kuna mambo mazuri yanakuja kutoka kwa Tunda Man,” alisema Tunda.
Pia muimbaji huyo amesema bado hajajua ni wimbo upi utaanza kutoka kati ya ‘Mwanaume Suruali’ pamoja na wimbo wa hiyo kolabo yake na Jaguar.
Wimbo wa ‘Mwanaume Suruali’ ameshindwa kuuachia hivi karibuni baada ya video ya wimbo huo kuzuiliwa kutokana na kumtumia video queen ambaye ni mke wa mtu
Kukanusha kwa taarifa zilizoenea kuhusu ajira Serikalini
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira anapenda kuwataafu wadau na wananchi wote kwa ujumla kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote na inalenga kuupotosha Umma, hivyo wananchi wote wanapaswa kuzipuuza.
Matangazo yote ambayo hutolewa na Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni lazima yaonekane kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz au portal ya Ajira ambayo ni portal.ajira.go.tz.
Mahakama yabariki urais wa Nkurunziza
Uamuzi huo ulitolewa na Mahakama ya Katiba ya Afika Mashariki (EACJ) kutokana na kesi iliyofunguliwa dhidi yake na asasi tatu za kiraia za Burundi, ambazo zilidai amejiongezea muda wa uongozi kinyume cha katiba.
Kupingwa kwa Rais Nkurunziza kuendelea kuwa rais kwa awamu tatu, kulisababisha kuibuka jaribio la kumpindua Mei, mwaka jana, chini ya Meja Jenerali Godefroid Niyombane.
Kutokana na kuongoza jaribio hilo, Meja Jenerali Niyombane alitimuliwa ukuu wa usalama, ikiwa miezi mitatu baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Mapema nchini humo, Mahakama ya Katiba ilimthibitisha Nkurunziza baada ya uteuzi wa chama chake cha CNDD FDD kumpitisha kupeperusha bendera katika uchaguzi mkuu.
Hukumuiliyosomwa jana na Jaji Isack Lenaola, ilithibitisha uhalali wa Rais Nkurunziza kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa awamu ya tatu kwa mujibu wa Katiba.
Taasisi 9 za serikali zakutwa na viashiria vya rushwa
Taasisi tisa za serikali ikiwamo Taasisi ya Mifupa (MOI), Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, zimetajwa kuwa na viashiria vya rushwa.
Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma(PPRA) Matern Lumbanga.
Maeneo matano yaliyoangaliwa ni ukidhi wa sheria ya manunuzi ya umma, ukiukwaji wa sheria na taratibu za manunuzi, kupima thamani halisi ya fedha ilivyotumika, malipo yenye utata na viashiria vya rushwa.
Wenger: Wachezaji wa Afrika wamenifaa sana katika soka
Wenga alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wake wa kawaida na waandishi wa habari kabla ya mechi ambapo pia alitunukiwa kwa kukiongoza klabu hicho kwa miongo mwili.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh. Geoffrey Idelphonce Mwambe amewasimamisha kazi watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mh. Geoffrey Idelphonce Mwambe amewasimamisha kazi watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao vizuri, uzembe na utovu wa nidhamu.
Mwambe
amefanya uamuzi huo alipokuwa kwenye Mkutano na Wafanyakazi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni leo Tarehe 29.09.2016, ambapo aliwataja
Watumishi hao aliowasimamisha kazi kuwa ni Mkuu wa Idara ya Ugavi Bw.
Genesius Rugemalira ambaye amesimamishwa kwa kushindwa kusimamia
manunuzi ya Halmashauri na kuisababishia Serikali hasara ya Tshs. Mil
16, Daktari John Amita wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni aliyesimamishwa
kazi kwa tuhuma za kupigana na daktari mwenzake hospitalini hapo,
tuhuma za utoaji mimba, na uzembe uliopelekea kifo cha mama mjamzito.
Wengine
waliosimamishwa ni Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni Bw. Mika
Iloti kwa uzembe uliopelekea kifo cha Mama mjamzimzito, Msaidizi wa
Ofisi Bw. Anthony Sanga kwa ufujaji wa mapato ya Halmashauri na Mtendaji
wa Kijiji cha Makasuku Bw. Mussa Ndahani ambaye kwa kushirikiana na
Mwenyekiti wa Kijiji chake wamekuwa wakitoa vibali vya uvunaji Misitu
kwa Wafanyabiashara ya mbao bila kuzingatia sheria na taratibu kwa kofia
ya zoezi la utengenezaji wa madawati linaloendelea.
Mh.
Mwambe amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni
kuhakikisha Watumishi hao wanasimamishwa mara moja kupisha uchunguzi wa
tuhuma zinazowakabili ili hatua Zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Viongozi mbalimbali wahudhuria mazishi ya waziri mkuu wa zamani wa Israel, Shimon Peres
Viongozi wa dunia wamehudhuria mazishi ya waziri mkuu na rais zamani wa Israel, Shimon Peres.
Mazishi hayo yamegubikwa na ulinzi mkali.
Orodha kubwa ya viongozi wa mataifa mengine uliwasili kwaajili ya kutoa heshima zao za mwisho.
Wapo Rais wa Marekani, Barack Obama, Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, Waziri wa mambo ya nje wa Misri, Sameh Shoukry na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani.
Askari wakiwa wamelibeba jeneza la mwili wa Shimon Peres
Rais Barack Obama akisalimiana na wageni
Pluijm: Simba, Maneno Yenu Yote Mwisho Kesho
Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm.
Katika mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Simba, Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amesema imetosha kuhusiana na vita ya maneno inayoendelea kati yao na kinachofuata atawanyamazisha wapinzani kwenye mechi yao hiyo.
Pluijm ameeleza zaidi kuwa wakati mwingine haifai kuongea maneno mengi kuelekea katika mchezo huo kwa kuwa kikosi chake
kinafahamu nini cha kufanya ili kunyamazisha maneno yote yanayoendelea mitaani kuanzia kwa mashabiki, wapenzi, wadau mpaka viongozi.
“Huu mchezo umewaweka wengi kwenye presha, sasa sitaki kuongea sana, kuna maneno mengi yameshaongelewa na hii ni kwa kuwa ni mchezo wenye presha kwa sababu ni moja ya utani wa jadi uliopo, sasa kwa upande wetu nadhani hatuhitaji kuongea zaidi ya kufanya kazi hiyo Jumamosi.
“Wachezaji wangu wanafahamu mashabiki wanataka nini na nini cha kufanya kuzima hii presha iliyopo kwa mashabiki na wapenzi wengi wa Yanga, kumeshakuwa na maneno mengi lakini sasa ni vizuri kukaa
NSSF,mkoa wa Arusha,umezifikisha taasisi Nne mahakamani,kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao
Ahmed Mahmoud- Arusha
MFUKO wa hifadhi ya jamii NSSF,mkoa wa Arusha,umezifikisha taasisi Nne mahakama ya hakimu mkuu mkazi Arusha,kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa vipindi tofauti zaidi ya shilingi bilioni moja.
Mwanasheria
mwandamizi wa NSSF, Selestini Ntagale, ameiambia mahakama ya hakimu
mkuu mkazi kuwa taasisi hizo zimeshindwa kuwasilisha malimbikizo ya
michango ya wafanyakazi hao kwenye mfuko huo licha ya kukumbushwa mara
kwa mara.
Aliiambia
mahakama hiyo kuwa michango ni haki ya mfanyakazi lakini kampuni hizo
zimekuwa zikiwakata kwenye mishahara na haziwasilishi michango hiyo
hivyo NSSF,kulazimika kutumia sheria kwa kuzifikisha mahakamani ili
mahakama iziamuru kuwasilisha michango hiyo.
Miongoni mwa kampuni hizo ni pamoja na ,Water Solution, Net Health, na Hotel ya Snow Crest zote za Arusha.
Ntagale,
aliiambia mahakama hiyo kuwa Kampuni ya Pride Tanzania, tayari ndani ya
siku mbili imeshalipa shilingi milioni 180 kati ya deni lake la milioni
709 .
Ntagale,
alisema Hotel ya Snow Crest inadaiwa tangia mwaka 2015 ambapo
imechelewa kutekeleza hukumu iliyotolewa na hakimu mkazi na hivyo NSSF
kukaza hukumu ambapo kama itashindwa kutekeleza NSSF itaomba kibali cha
mahakama cha kuiuza hotel hiyo kwa njia ya mnada ili kulipwa malimbikizo yanayodaiwa.
Aidha taasisi zingine zikiwemo Water Solution inadaiwa shilingi milioni 83.143.813,Hotel
ya Snow Crest inadaiwa shilingi 449 na Net Health, inadaiwa shilingi
milioni 14, 743,376,madeni ambayo ni malimbikizo yanayotokana na makato ya mishahara ya wafanyakazi ambayo hayajawasilishwa NSSF.
Wakili
mwandamizi, Method Kimomogoro, ambae anaiwakilisha kampuni ya Pride
Tanzania, ameaiambia mahakama kuwa wateja wake wanakubaliana na deni
hilo na watalilipa ndani ya mwezi mmoja .
Kimomogoro, aliiambia mahakama kuwa mteja wake amepewa muda mfupi wa siku mbili na
baada ya kupata taarifa hiyo wamelipa kiasi hicho cha fedha hivyo
anaomba apewe muda wa mwezi mmoja hadi Novemba 4 wawe wamemaliza kiasi
kilichobakia.
Katika hatua nyingine mahakama imetoa hati
ya kukamatwa kwa kampuni ya Net Health, ambayo haikufika mahakamani
hapo huku kampuni ya Water Solution imeyakataa madai hayo ya NSSF
wakidai sio sahihi .
Akiahirisha
kesi hiyo, hakimu mkuu mkazi, Augostino Rwizila, amewataka wadaiwa wate
kulipa madeni yao ndani ya muda wa mwezi mmoja ambapo ameahirisha kesi
hiyo hadi Novemba 4 mwaka huu.
Kwenye kesi hiyo kila mdaiwa ana kesi yake binafsi kulingana na madeni yake ingawa zote zinasikilizwa na hakimu mmoja .
Kesi
hizo ni kama ifuatavyo, Net Health kesi namba, 389/ 2016, Pride
Tanzania limited, kesi namba, 388/ 2016, Water Solution kesi namba, 390/
2016 na Hotel ya Snow Crest kesi namba 61/ 2015 .
Kikosi cha Taifa stars
Kocha Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi ambacho kitasafiri mwishoni mwa wiki ijayo kwenda Addis Ababa, Ethiopia kucheza na wenyeji wetu kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Oktoba 8, mwaka huu.
Mkwasa maarufu kwa jina la Master amesema wachezaji aliowaita wataingia kambini Oktoba 2, 2016 kabla ya kuanza kukiandaa kuanzia Oktoba 3, 2016 ikiwa mara baada ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii ambako Mwadui itacheza na Azam huku Mbao ikishindina na JKT Ruvu Oktoba 2, mwaka huu.
Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni hawa
Makipa
Deogratius Munishi – Young Africans
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC
Mabeki
Shomari Kapombe – Azam FC
Juma Abdul – Young Africans
Vicent Andrew – Young Africans
Mwinyi Haji – Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
David Mwantika – Azam FC
James Josephat – Tanzania Prisons
Viungo wa Kati
Himid Mao – Azam FC
Mohammed Ibrahim – Simba SC
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Viungo wa Pembeni
Shiza Kichuya – Simba SC
Simon Msuva – Young Africans
Juma Mahadhi – Young Africans
Jamal Mnyate – Simba
Hassan Kabunda – Mwadui FC
Washambuliaji
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco – Azam FC
Mbwana Samatta – CK Genk ya Ubelgiji
Elius Maguli – Oman
Thomas Ulimwengu – TP Mazembe Congo
Mchezo huo utakaofanyika jijini Addis Ababa, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia (EFF), wameo
Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana kina alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.
Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Ethiopia yenyewe inashika nafasi ya 126.
Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Ujerumani, Colombia na Brazil.
Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 34 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Algeria, Senegal, Tunisia na Ghana.
Wastara apata shavu la ubalozi wa kampuni mpya ya simu
Wastara akionyesha mkataba
Malkia wa filamu Wastara Juma amepata shavu la kuwa balozi wa
kampuni ya simu za mkononi ya KZG Tanzania yenye makao makuu yake nchini
China.
Katika mkataba huo mwigizaji huyo atavuna kiasi cha tsh milioni 400 kwa
miaka miwili akiwa balozi wa kampuni hiyo kwa matangazo na matamasha
mbalimbali.Akiongea na Filamu Central meneja mauzo wa kampuni ya KZG Tanzania, Raymond Kalikawe amesema kuwa kamapuni yao imelenga kusambaza teknolojia vyuoni kwani wana bidhaa nyingi ambazo zinatumika katika kufundishia wanafunzi hao.
“Leo pia tunazindua simu ya kipekee kabisa kufika hapa nchini Kzg Kimi ambayo inatumia betri ya ndani kwa ndani ambayo ina sifa ya kutengenezeka tofauti na zingine ambazo betri zake zikiharibika hazitengenezeki,”alisema Kalikawe.
Pia Wastara ameishukru kampuni hiyo kwa kumwamini na kutambua kuwa ana vigezo stahili kuwa balozi wao na kuahidi kuwa hatowaangusha katika kuitangaza kampuni hiyo sambamba na bidhaa zake zilizalishwazo na kampuni hiyo ambayo utengeneza simu, Computer na vifaa vingine vya teknolojia.
Uzinduzi huo ulisindikizwa na wasanii wa Bongo movie wakimpongeza Wastara kuingia mkataba huo.
Thursday, 29 September 2016
Pato la Taifa limekua kwa jumla ya thamani ya Shilingi trilioni 11.7
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa taarifa ya Pato la Taifa Robo
ya Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka 2016 kwa waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za
Uchumi wa ofisi hiyo Bi. Joy Sawe. Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Pato la
Taifa limekua kwa kasi ya asilimia 7.9 katika kipindi cha mwezi Aprili
hadi Juni 2016 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.8 katika kipindi
kama hicho mwaka 2015.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa taarifa ya Pato la Taifa Robo
ya Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka 2016 kwa waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa
wa Ofisi hiyo Daniel Masolwa. Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Pato la Taifa
limekua kwa kasi ya asilimia 7.9 katika kipindi cha mwezi Aprili hadi
Juni 2016 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.8 katika kipindi kama
hicho mwaka 2015.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina
Chuwa (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya Pato la Taifa Robo ya
Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka 2016 leo jijini Dar es Salaam. Taarifa
hiyo imeonyesha kuwa Pato la Taifa limekua kwa kasi ya asilimia 7.9
katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni 2016 ikilinganishwa na kasi ya
asilimia 5.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2015. (PICHA NA EMMANUEL GHULA)
Na Veronica Kazimoto-Dar es Salaam
Pato la Taifa limekua kwa jumla
ya thamani ya Shilingi trilioni 11.7 katika kipindi cha robo ya pili ya
mwaka 2016 ikilinganishwa na Shilingi trilioni 10.9 katika kipindi kama
hicho cha mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema ukuaji wa pato la Taifa
umetokana na shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo, mifugo, misitu na
uvuvi ambapo shughuli hizo zimekuwa kwa asilimia 3.2 ikilinganishwa na
ukuaji wa asilimia 1.9 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Kwa upande wa shughuli za
uchumi za viwanda na ujenzi, Dkt. Chuwa alisema kumekua na ongezeko la
asilimia 20.5 katika kipindi hicho ukilinganisha na ukuaji wa asilimia
11.2 mwaka 2015 katika shughuli za uchimbaji madini, mawe na kokoto.
Aidha shughuli za uzalishaji
bidhaa na viwanda zimeongeza kwa asilimia 9.1 katika kipindi cha robo ya
pili ya mwaka 2016 ukilinganisha na kasi ya asilimia 5.2 ya mwaka 2015.
Shughuli za uchukuzi na
uhifadhi, Dkt. Chuwa amesema kuwa shughuli hizo zimekua kwa kiwango cha
asilimia 30.6 zikisababishwa na usafirishaji wa abiria kwa njia ya reli
na barabara ikiwa ni pamoja na usafiri wa UDART.
Vilevile, shughuli za fedha na
bima zimeongezeka kwa kasi ya asilimia 12.5 ikilinganishwa na asilimia
10.0 iliyopatikana katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Dkt. Chuwa amefafanua kuwa
huduma za elimu zimekua kwa kasi ya asilimia 8.0 katika robo hiyo ya
mwaka ikilinganishwa na aslimia 7.4 ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2015
ambapo ukuaji wa shughuli hii imetokana na ongezeko la wanafunzi
waliodahiliwa mwaka 2016.
Kwa upande wa Nchi za Afrika
Mashariki ambazo zimeshachambua na kutoa Pato la Taifa katika kipindi
kinachoishia Juni 2016 ni Rwanda ambapo Pato halisi la Nchi ya Rwanda
katika kipindi cha Aprili – Juni 2016 limeendelea kukua kwa asilimia 5.4
ikilinganisha na asilimia 7.2 ya miezi kama hiyo mwaka 2015.
Bomba la mafuta lalipuliwa Nigeria
Kumwagika kwa mafuta kumechafua mazingira nchini Nigeria
Kundi la waasi katika eneo lenye utajiri wa mafuta nchini Nigeria
linasema kuwa limelipua bomba la mafuta kama sehemu ya kampeni yenye
kichwa "tunamiliki ardhi zetu."Afisa wa idara ya ujasusi nchini Nigeria, aliliambia shirika la habari la AFP kuwa bomba hilo lililipuliwa na kundi la waasi
Bomba hilo liko chini ya usimamizi wa kampuni ya Nigeria Petroleum Development , sehemu ya kampuni ya serikali ya Nigeria Petroleum Corporation.
Eneo hilo lenye utajiri wa mafuta la kusini mwa nchi, limeshuhudia mashambulizi tangu Rais Muhammadu Buhari ambaye anatoka kaskazizi aingie madarakani mwaka uliopita.
Waasi wanataka wapewe mgao wa utajiri wa mafuta na pesa kutoka kwa mauzo ya mafuta kutumiwa kupambana na umaskini eneo hilo. Aidha wametaka kumalizika kwa uchafuzi unaosababishwa na sekta ya mafuta.
Samatta uwanjani leo kuiongoza Genk Vs Sasuolo
Mechi hiyo ya Kundi F katika michuano ya Europa itakuwa ni hatua nyingine KRC Genk kujiweka vizuri katika michuano hiyo.
Samatta, alikosa michezo miwili iliyopita kwenye ligi kwa sababu ya majeruhi, lakini anarudi uwanjani kutaka kuisaidia klabu yake, iliyopoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Rapid Wien.
Genk endapo itashinda mchezo wa leo, itajiweka mazingira mazuri kupigania kutinga 16 bora, katika kundi F.
Serikali yatenga Bilioni100 ukarabati wa viwanja vya ndege
Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dk John Magufuli imetenga kiasi cha sh. Bil. 100
katika bajeti ya mwaka 2016/17 kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa
viwanja mbalimbali vya ndege nchini.
Rais Dk. Magufuli alisema hayo
juzi katika sherehe za uzinduzi wa ndege mbili za Shirika la ndege la
Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Dash 8 Q400 zilizonunuliwa na
serikali, kwenye Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), ambapo viwanja hivyo vitaboreshwa ili kuwezesha ndege hizo kutua
bila wasiwasi.
Mhe. Rais akifafanua zaidi,
alisema , kiwanja cha ndege cha Nduli kilichopo umbali wa kilometa 13
Kaskazini Mashariki mwa Manispaa ya Iringa, ambacho kipo kwenye kiwango
cha lami kitakarabatiwa, ili ndege hizo zitue na kupaa bila tatizo.
Dk. Magufuli alisema, kiwanja cha
Nduli Iringa ni kiunganishi kikubwa na JNIA na kitatumika kupeleka
watalii wanaokwenda kutembelea mbuga ya wanyama ya Ruaha, wakitokea
Mataifa mbalimbali duniani.
Alisema mbali na kiwanja hicho
cha Nduli, pia kiwanja cha Musoma kitawekwa lami, ili nacho kiwe moja ya
maeneo ndege hiyo itakwenda, na kurahisisha usafiri wa watalii
watakaokwenda kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti. Kwa sasa kiwanja cha
Musoma kipo katika kiwango cha changarawe na kinatumika kwa ndege
mbalimbali kutua na kupaa.
Kwa mujibu wa Meneja wa Kiwanja
cha ndege cha Nduli, Bi. Hannah Kibopile, kiwanja hicho kinapokea ndege
ndogo zaidi ya saba zenye uwezo wa kubeba abiria 13, na kati ya hizo
tatu zipo kwenye ratiba maalum ya kila siku na zilizosalia ni za
kukodishwa na nyingine zinakwenda mbuga ya wanyama ya Ruaha.
Bi. Kibopile alisema ndege zinazotua kwenye kiwanja hicho zinatoka Jijini Dar es Salaam, Sumbawanga, Songea na Mbuga ya Ruaha.
Naye Kaimu Meneja wa Musoma, Bi.
Faraja Mayugwa amesema kiwanja hicho kinapokea ndege zaidi ya nne kwa
siku na nyingi zinakuwa za kukodi zinazopeleka watalii mbugani.
Katika hotuba yake, Rais Magufuli
alisema “Hii ndege inaweza kutua katika kiwanja cha aina yeyote; na
serikali itaendelea na ukarabati wa viwanja vya ndege vya pembezoni, ili
viwe katika kiwango, ambacho ndege hizi zitatua na kuruka bila
wasiwasi,”.
Akifafanua zaidi Dk. Magufuli
alisema serikali inatarajia kununua ndege nyingine kubwa mbili zenye
uwezo wa kubeba abiria 160 na 242, ambazo zitaanzia safari zake kwenye
JNIA kwenda sehemu mbalimbali duniani kama China au Marekani moja kwa
moja, ikiwa ni lengo la kupata abiria hao, ambao wengi wao watakuwa
watalii wanaokuja nchini kutembelea vivutio mbalimbali. Bombardier
inauwezo wa kubeba abiria 76.
Naye Waziri wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof Makame Mbarawa awali wakati
akimkaribisha Mhe. Rais kuzungumza na wananchi katika ghafla hiyo ya
uzinduzi wa ndege, alisema kwa kuanzia ndege hizo zitatua kwenye viwanja
11 vya ndege, ambavyo ni Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), Kilimanjaro (KIA), Zanzibar (AAKIA), Mwanza, Dodoma, Arusha,
Bukoba, Kigoma, Tabora, Mbeya na Mtwara. Pia ndege hiyo itakwenda
Comoro.
Mhe. Prof. Mbarawa ameiagiza
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuendelea kufanya upembuzi
yakinifu kwa kuangalia viwanja vingine vya ndege, ambavyo ndege hizi
zitakwenda.
Manispaa ya Temeke yagawanywa ni baada ya wilaya ya Ubungo na Kigamboni kuongezeka
Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo.
Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo amesema Halmashauri ya Manispaa
ya Temeke hivi sasa inagawanywa rasmi hali itakayowagawanya madiwani wa
kata za eneo hilo pia.Chaurembo akiwa katika tukio hilo leo, alisema mgawanyo huo umetokana na hatua ya serikali kuongeza wilaya za Ubungo na Kigamboni na kusema kuwa baadhi ya madiwani watabaki Temeke na wengine watakwenda Kigamboni.
Kwa sasa manispaa ya Kinondoni imeshagawanywa na kata 20 kati ya 34 zimebaki Kinondoni na kata 14 zipo Ubungo.
Taarifa ya CUF tawi chuo kikuu cha Mlimani
WITO KWA WANACUF
Chama cha wananchi C.U.F tawi la Chuo Kikuu UDSM kinapenda kuwajulisha wanacuf kuwa Ijumaa Septemba 30 wajumbe wa BARAZA KUU na WABUNGE wa C.U.F watawasili ofisi kuu za C.U.F taifa zilizopo BUGURUNI JIJINI DSM.
Katika msafara huo viongozi wakuu wa chama watakuwepo wakiwemo Katibu Mkuu taifa MAALIM SEIF SHARIFU AHMAD, mwenyekiti wa kamati ya uongozi CUF Mh JULIUS SUNDAY MTATIRO na viongozi wengine waandamizi wa chama.
Hivyo, Chama cha Wananchi CUF tawi la chuo kikuu cha DSM kinawaomba wanacuf wote kujitokeza kwa wingi mapema asubuhi kwenye ofisi hizo za BUGURUNI tayari kwa kufanya mapokezi makubwa ya viongozi hao wa chama ambao wanawasili ofisini hapo kwa lengo kuu la kupanga mikakati ya kukijenga chama.
Tunawaomba wanachama wote, vijana, wazee , akina mama, wanachuo wa CUF na wapenzi pamoja na wakereketwa wote wazalendo wa CUF kujitokeza kwa wingi wakiwa na vipeperushi vya chama, sare na kila aina ya vitu vyenye kuashiria upendo wa viongozi wetu wa CUF.
TUNAWAKARIBISHA WANACUF WOTE MAKAO MAKUU BUGURUNI KWA MAPOKEZI.
CUF ILIJENGWA NA WANACUF, IMEJENGWA NA WANACUF, INAJENGWA NA WANACUF NA ITAJENGWA NA WANACUF.
TUNAWATAKIA MAANDALIZI MEMA YA MAPOKEZI.
HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa na :-
Mwl Razaq Mtele Malilo.
Katibu CUF vyuo vikuu tawi la Mlimani-UDSM.
Profesa Tibaijuka akataa zaidi ya Sh 200 milioni za tuzo
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anne Tibaijuka.
. Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anne Tibaijuka
amesema amepata tuzo nchini Marekani ikiwa ni kuthamini mchango wake
akiwa Umoja wa Mataifa lakini akakataa kuchukua fedha dola 100,000(
zaidi ya Sh 200 milioni) ambazo huambatana na tuzo hiyo.
Trump apoteza $800m kipindi cha mwaka mmoja
Mfanyabiashara tajiri wa New York anayewania urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amepoteza $800m ya utajiri wake katika kipindi cha mwaka mmoja, kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Jarida hilo linasema kwa sasa utajiri wa Bw Trump ni $3.7bn (£2.7bn).
Forbes wanasema kushuka huko kwa thamani ya utajiri wake kunatokana na 'kudorora kiasi' kwa biashara ya nyumba na ardhi katika soko la New York.
Bw Trump, ambaye wakati mmoja liandika kitabu kwa jina Midas Touch (Mguso wa Midas: Midas aliaminika kubadilisha kila alichogusa kuwa dhahabu), amekuwa akisema kwamba rais wa Marekani kwa sasa anaweza kuwa mtu mwenye busara katika biashara na majadiliano.
Wakati wa mdahalo wa urais Jumatatu, alisema: "Nina mapato makubwa ... wakati umefika kwa taifa hili kuwa na mtu anayefahamu mengi kuhusu pesa."
Alipoteza vipi $800m?
Forbes, ambao wamekuwa wakikadiria utajiri wa Bw Trumo kwa zaidi ya miongo mitatu, wanasema hilo limetokana na kudorora kwa soko la nyumba, afisi na ardhi New York.
Kati ya majumba 28 ambayo yalichunguzwa na Forbes, 18 yalishuka thamani, likiwemo jumba maarufu la Trump Tower linalopatikana Manhattan.
Jumba lake lililo 40 Wall Street na kilabu chake cha Mar-a-Lago kilichopo Palm Beach, Florida, pia vilipoteza thamani, kwa mujibu wa Forbes.
Lakini majumba saba ya Trump, likiwemo jumba la pili kwa urefu San Francisco, yalipanda thamani.
Ametumia pesa ngapi kwenye kampeni?
Forbes wanakadiria kwamba matamshi yake dhidi ya wahamiaji wa Mexico yalimgharimu $100m kupitia mikataba aliyopoteza kwenye mashirika makubwa kama vile NBC Universal, Univision na Macy's.
Ivana na Donald Trump mwaka 1989
Utajiri wake kamili?Utajiri wake kamili haujulikani. Alipowasilisha taarifa zake za kifedha kwa Tume ya Dola ya Uchaguzi, alisema ana "zaidi ya dola bilioni kumi."
Lakini Forbes wanasema utajiri wake ni $3.7bn, Bloomberg wanasema anamiliki $3bn nao Fortune wanasema ana $3.9bn.
Moja ya sababu inayochangia hili ni kwamba Bw Trump pia huhesabu thamani ya jina lake, ambalo anakadiria kwamba thamani yake ni karibu $3.3bn.
Marekani yazuilia mali ya maafisa wawili wa DR Congo
Jenerali John Numbi, (kushoto) akiwa na Jenerali Christian Damay wa
jeshi la Ufaransa baada ya kikao na wanahabari mjini Kinshasa 14 Julai
2006.
Serikali ya Marekani imetangaza kwamba itazuilia mali ya maafisa wawili wakuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Marekani inawatuhumu wawili hao, mkuu wa zamani wa polisi Jenerali John Numbi na afisa mkuu wa jeshi Meja Jenerali Gabriel Amisi ajulikanaye kwa majina ya utani kama Tango Fort au Tango Four kwa kuwa "tishio kwa uthabiti na kuhujumu shughuli za kidemokrasia".
Wizara ya fedha ya Marekani imesema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kuzidi kwa vitendo vya ukandamizaji dhidi ya wapinzani, sana kwa kutumia nguvu.
Kwa mujibu wa kituo cha redio cha Virunga Business, ingawa Jenerali Amisi bado anahudumu, John Numbi hajatekeleza majukumu rasmi kwa miaka mingi tangu kuuawa kwa mtetezi wa haki za kibinadamu Floribert Chebeya. Jenerali Numbi alisimamishwa kazi Juni 2010 baada ya kifo cha mwanaharakati huyo.
"Maafisa hawa wa serikali ya DR Congo wamejihusisha katika vitendo vya kuhudumu shughuli za kidemokrasia na kukandamiza haki za kisiasa na uhuru wa watu wa Congo, na kuzidisha hatari ya kuenea kwa ukosefu wa uthabiti DR Congo na eneo lote la Maziwa Makuu," kaimu mkurugenzi wa idara inayoangazia mali ya raia wa nje ya Marekani John Smith amesema kupitia taarifa.
Miezi minne iliyopita, mkuu wa polisi wa Kinshasa Celestin Kanyama pia aliwekewa vikwazo.
Bw Numbi anatoka Kolwezi, mkoa wa Katanga na anadaiwa kutumia nguvu na kuwatisha wapinzani wakati wa uchaguzi wa majimbo uliofanyika Machi 2016.
Anadaiwa kutishia kuua wapinzani wa wagombea wanaomuunga mkono Rais Joseph Kabila iwapo hawangejiondoa. Wagombea watatu wanadaiwa kujiondoa kutokana na vitisho hivyo.
"Ingawa si afisa wa serikali ya DR Congo tena, Numbi bado anaaminika kuwa mshauri wa Rais Kabila mwenye ushawishi mkuu," taarifa ya Marekani imesema.
Jenerali Amisi, ajulikanaye pia kama Tango Fort
Jenerali Amisi anadaiwa kuwa kiongozi wa kundi la kijeshi linalosimamia
mikoa ya Bandudu, Bas Congo, Equateur na Kinshasa, ambao walitumiwa
kuzima maandamano ya kisiasa, hasa yaliyoandaliwa na upinzani na
mashirika ya kiraia Januari 2015.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa watumishi waliohamishiwa wilaya mpya ya Kibiti mkoani Pwani kuripoti katika vituo vyao
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
ametoa mwezi mmoja kwa watumishi waliohamishiwa wilaya mpya ya Kibiti
mkoani Pwani kuripoti katika kituo chao cha kazi na watakaoshindwa
kutekeleza watakuwa wamejifukuzisha kazi.
Amesema mtumishi yeyote
aliyehamishiwa wilaya hiyo ambaye anaishi nje ya Kibiti anatakiwa arudi
na kuishi kwenye makao makuu ya wilaya na si vinginevyo.
“Tayari nimemuagiza ndugu Zuberi
Samatabu Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani kuhakikisha anasimamia
watumishi wote wa wilaya hiyo wanaoishi nje ya wilaya hiyo waishi
Kibiti na si Ikwiriri,” amesema.
Kauli hiyo ya Waziri Mkuu
ilifuatia taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo
Alvera Ndabagoye ambaye alimueleza Waziri Mkuu kuwa ni watumishi wanane
pekee kati ya 74 waliopangiwa kufanya kazi kwenye wilaya hiyo
wameripoti katika kituo cha kazi
Ili kukabiliana na tatizo la
uhaba wa nyumba za watumishi amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo kuzungumza na watendaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii
kwenda wilayani huko kuwekeza katika miradi ya ujenzi wa nyumba za
watumishi.
Serikali imetoa shilingi milioni 17 na kampuni ya simu ya Halotel imetoa shilingi milioni 15 kwa waathirika wa tetemeko Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja
Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiongea na wawakilishi wa familia
waliopoteza ndugu zao (hawapo pichani) kwa tetemeko la ardhi lililotokea
mapema Septemba 10 mwaka huu Bukoba mjini wakati wa kukabidhiwa
rambirambi iliyotolewa na Serikali milioni 17 pamoja na kampuni ya simu
ya Halotel ambayo imetoa shilingi milioni 15.kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Maafa
Yusta Jonas mkazi wa Hamugembe
Manispaa ya Bukoba akipokea rambirambi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ambayo imetolewa na Serikali pamoja
na kampuni ya simu za mkononi ya Halotel.
Mzee Vedasto Kato kutoka mtaa wa
Hamgembe Manispaa ya Bukoba akipokea rambirambi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ambayo imetolewa na Serikali
pamoja na kampuni ya simu za mkononi ya Halotel.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja
Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (katikati aliyekaa) akiwa katika picha ya
pamoja na wawakilishi wa wanafamilia waliofiwa na ndugu zao wakati wa
tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, mwaka huu.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba)
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba
Familia 15 zilizofiwa na ndugu
zao 17 wakati wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani wa Kagera
zimepokea rambirambi ya jumla ya shilingi milioni 32 ikiwa ni mkono wa
faraja kwa msiba uliwafika familia hizo na taifa kwa ujumla.
Rambirambi hiyo imetolewa mjini
Bukoba na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kwa
niaba ya Serikali kwa kushirikiana na kampuni ya simu za mkononi nchini
ya Halotel ili kuwashika mkono wafiwa hao kwa kupoteza ndugu na jamaa
zao.
Katika rambirambi hiyo, Serikali
imetoa shilingi milioni 17 na kampuni ya simu ya Halotel imetoa shilingi
milioni 15 ambapo kila familia ya mfiwa amepokea shilingi 1,000,000
kutoka Serikalini na shilingi 885,000 kutoka kampuni ya Halotel.
Hatua hiyo inapelekea kila
familia ya mfiwa kupokea jumla shilingi 1,885,000 ambapo familia mbili
zilizopoteza ndugu zao wawili wawili wamepokea jumla ya shilingi
3,770,000 ikiwa ni rambirambi kwa kila ndugu aliyefariki wakati wa tukio
hilo la tetemeko la ardhi.
Akikabidhi rambirambi hiyo kwa
familia hizo, Mkuu wa Mkoa wa huo akiwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya
Maafa mkoa Meja Jenerali Mstaafu Kijuu amesema kuwa Serikali imetoa
rambirambi hiyo kwa lengo kuwapa pole wafiwa hao kutokana na kuwapoteza
ndugu na jamaa zao wakati wa tetemeko hilo lililotokea Septemba 10,
mwaka huu.
Airtel na Puma washirikiana kununua mafuta kwa kutumia huduma ya Airtel Money Tap Tap
MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti kushoto na Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso wakibadilishana mikataba
mara baada ya kuasini makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi
ya Aiter Money Tap Tap , Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta
cha Puma Oysterbay.
MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti kushoto na Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso wakiasini mkataba wa
makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi ya Aiter Money Tap Tap ,
Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay jijini
Dar es salaam.
Baadhi ya maofisa wa Puma na
Aiter wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye kituo cha mafuta cha
Puma Oysterbay jijini Dar es salaam.
Meneja Rasilimali Watu wa Puma
Tanzania Bi Loveness Hoyange pamoja na maofisa wengine wa kampuni hiyo
na kampuni ya Kampuni ya simu ya Aitel wakifuatilia matukio katika hafla
hiyo.
Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matindekulia na baadhi ya maofisa wa kampuni ya Aitel na Puma wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso kulia na
MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti wakishuhudia
wakati mmoja wa wateja wa Aitel Money na Puma akijaziwa mafuta kwa
kutumia huduma ya Airtel Money Tap Tap katika kituo cha mafuta cha Puma
Oysterbay jijini Dar es salaam.
Meneja Mkuu wa Puma Energy
Tanzania Philippe Corsaletti amesema wanalo jukumu la kuhakikisha
huduma wanazitoa kwa ajili ya Watanzania zinakuwa salama wakati wote
ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za
kuhamasisha kutumia njia za kieletroniki kwenye malipo ya fedha.
Corsaletti alitoa kauli hiyo
Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa huduma mpya inayojulikana kwa
jina la Airtel Money Tap Tap ambayo inamuwezesha mteja wao anapotaka
kununua mafuta kwa kutumia kadi ya Airtel badala ya kutoa fedha taslimu
akiwa kituo cha mafuta.
Alisema wanahisi kwamba
wanawajibu wa kufanya huduma zao kwa usalama, senye ufanisi na rahisi
zaidi kwa wateja wao na kufafanua ni hatari kubeba fedha wakati wote
maana ni rahisi kuhatarisha maisha.
Aliongeza hivyo ili kufanya
jamii ya Watanzania inakuwa salama wakati wote imeona kuna haja ya kuwa
na huduma hiyo ambayo itamuwezesha anayehitaji kununua mafuta kwenye
vituo vya Puma vilivyopo maeneo mbalimbali ya Dar es salaam wanatumia
kadi za Airtel kununua mafuta.
“Milango yetu iko wazi kwa
ajili ya kuendelea kuboresha huduma zetu na kuna jambo lolote ambalo
tunaweza kulifanya ili jamii yetu kuwa salama wakati wote.Hivyo kuna
umuhimu wa kuwa na matumizi ya kadi ya Airtel katika kununua mafuta
kwenye vituo vyetu vya Puma,”alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu huduma
ya Airtel Money Tap Tap, Corsaletti alisema chini ya utaratibu huo mtu
yeyote aliyejisajili na huduma ya Airtel Money atakuwa na uwezo wa
kulipia bidhaa za Puma katika vituo vyake vyote nchini kwa kutumia kadi
ya huduma ya Airtel Tap Tap badala ya kutumia fedha kwa ajili ya
huduma kama hizo.
“Kadi hii imeundwa kwa namna
ambayo wakati wa kutumika kufanya malipo , hupunguza fedha kwa kiasi
cha malipo kutoka katika akaunti ya Airtel Money ya mnunuzi kwenda
kwenye akaunti ya muuzaji. “Kadi hii itakuwa inauzwa kwa bei ya Sh 2,
000 kwenye vituo vyote vya Puma Dar es Salaam na maduka yote ya Airtel
Tanzania .
Subscribe to:
Posts (Atom)