Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akitia saini kitabu cha Wageni alipotembelea Kata ya Mbweni
iliyopo Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya shughuli za upandaji mikoko
katika eneo hilo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akipanda mti aina ya mkoko katika fukwe za bahari ya hindi
katika eneo la Mbweni jijini Dar es Salaam. Upandaji huo wa mikoko ni
katika kuadhimisha wiki ya mazingira duniani, ambayo kilele chake ni
kesho
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akishirikiana kupanda miti ya mikoko na wakazi wa kata ya
Mbweni jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha siku ya
mazingira hapo tarehe 5 juni.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akifurahia jambo na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbweni ambao
walijumuika pamoja naye kupanda mikoko katika fukwe za Mbweni jijini Dar
es salaam.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya
kumaliza kupanda mikoko katika fukwe za bahari ya Hindi katika kata ya
Mbweni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba Ametoa wito kwa
Wananchi wa Kata ya Mbweni kutunza mazingira na kutoa kipaumbele kwa
mazingira. Aliyasema hayo wakati wa zoez la upandaji mikoko lilifanyika
katika fukwe za bahari ya Hindi zilizoko Mbweni.
Akiongoza Wananchi wa Kata hiyo
kupanda miche 5,000 ya mikoko , Waziri Mkamba alisititiza pia Wanafunzi
wa shule waliopo katika eneo hilo kupenda mazingira yao na kuyatunza ili
yawafae baadaye.
Wakisoma Risala yao , Wanawake wa
Mbweni walimuomba Waziri awasaidie kuwapatia vitendea kazi kwa ajili
ya kuhudumia mikoko pamoja na kumuomba awasaide kuwatatulia changamoto
wanazokutana nazo. Ikiwamo ya maafisa wa TRA kukata hovyo mikoko
wanapokua wanafanya doria katika fukwe zaMbweni.
Mwisho Waziri aliwahukuru
Wananchi wa Mbweni waliojitypkeza kujumuika naye katika zoezi hilo la
upandaji mikoko. Shuhuli za upandaji mikoko ni kuelekea maadhimisho ya
siku ya mazingira ambayo kilele chake ni tarehe 5 juni kila mwaka.
No comments:
Post a Comment