
KAMPUNI ya Hope Light Film
inayojishughulisha na uandaaji wa filamu,Documenti na shughuli
mbalimbali ambazo zinawiana na uchukuaji wa picha za mnato na video
imeunda group ambalo litaweka ukaribu baina ya wadau na mashabiki wa
filamu za Bongo Movie katika kujadiliana mambo mbalimbali katika
uendelezaji wa kazi za sanaa nchini.
Akitoa taarifa hiyo kupitia
mtandao wa kijamii wa Facebook,Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Ally
Njenje,alisema kuwa ameunda kundi la ALLY NJENJE FANS kupitia Whatsap na
Facebook ili kuwaleta pamoja wadau na mashabiki wa kazi za filamu za
bongo movie za hapa nchini pamoja na kuunganisha katika mzunguko wa
biashara kwa wao kama hope Light Film kutangaza kazi zao na kwa watu
wengine pia kutangaza biashara zao ambapo linakuwa kundi la
kubadilishana mawazo ya kujiinua kiuchumi lakini pia kusapotiana katika
suala zima la biashara.
“Ndugu zangu wadau wa Kampuni ya
Hope Light Film napenda kuwajuza kuwa nimeunda group la ALLY NJENJE FANS
ambalo linaweka karibu mashabiki wa kazi zetu na kwa sababu wewe ni
shabiki wangu nami pia ni shabiki wako ambapo katika kundi hili ni vyema
kila mtu ajitambulishe kwa kazi anayofanya ili tupeane fursa wenyewe
kwa wenyewe kwa mfano nikijua wewe unafanya biashara aina fulani basi
humu kaa ukijua kuna wateja wako mmoja wapo ni mimi Ally Njenje lakini
isiwe biashara hatarishi”Alisema Njenje
Aidha amesema kuwa watu wote
watakaojiunga na kundi hilo watapata fursa ya kuwa wa kwanza kuangalia
kazi za Hope Light Film na kwa wale wote watakaokuwa tayari kuisambaza
kwenye libraly zao au zilizokuwa karibu yao au kwa wateja wowote wale na
kwa mwanakundi yeyote atakayekuwa tayari kuchukua copy kadhaa ambazo
ataenda kuziuza kwa kila copy atakayouza kutakuwa na pesa yake ni
mwanakikundi na uwezo wake wa uchakarikaji katika uuzaji wa kazi hizo.
“Ndio maana nasema kuwa ukiwa
ndani ya kundi hili utakuwa wa kwanza kuona kazi zangu na kazi za Hope
Light Film ili uangalie uzuri wake na kuangalia wapi utapeleka kuuza
kazi hizo suala hili ni la hiyari sio shuruti kwa mwenye kuiona fursa
hii ya biashara ambayo itakusaidia wewe na mimi kupata faida katika
kundi hili anakaribishwa sana”Alisema Njenje
Aliongeza kwa kutoa nafasi kwa
mtu yeyote mwenye kuona ana kipaji na ana nia ya kushiriki katika
kampuni yake kama muigizaji na akaongeza kusema kuna nafasi nyingi sana
ambazo zinahitaji watu kama uandishi wa stori za filamu,upigaji wa picha
za mnato na jongefu,kuongoza filamu,kuwafanyia make up waigizaji pamoja
na kuwa mshauri katika uboreshaji wa utengezaji wa filamu za Hope Light
Film ili kutoa kazi bora.
“Kama unahisi ndozto zako ni
kuigiza na hayo niliyoainisha hapo juu ukiwa kama kijana au mtu wa rika
lolote nakukaribisha kwenye group hili ili tufahamiane na kusaidiana
katika kujikwamua kiuchumi na kimaisha pia nataraji siku za karibuni
kuanzisha academy ya kulea watoto na watu wakubwa katika kuwajenga
kisanaa kwa kuwa naamini mimi ni msaada mkubwa kwao nitajitolea kutoa
elimu ya uigizaji na kuwapa nafasi wewe,kijana wako au ndugu yako
aliyeunganishwa au kupata taarifa hii kupitia mtu aliyejiunga katika
group langu la Ally Njenje Fans kwa sababu umenipa thamani kubwa name
napaswa kukurudishia thamani hiyo”Alisema Njenje
Alimaliza kwa kutoa wito kwa watu
wote wenye kuona wanaweza kuchangamkia fursa hiyo wajitokeze mapema
kumtafuta kupitia mtandao wa facebook kwa jina la Ally Njenje au kwa
Whatsap namba yake 0713103521 na kutoa
angalizo kuwa katika kundi hilo heshima na maadili ya mtanzania
yazingatiwe kwa kuwa ni katika kundi hilo kutakuwa na watu wa rika
mbalimbali na kushauri watu kuacha tabia ya kufuatana inbox kuelezana
mambo ya kijinga wengi wao katika kundi hilo wana ndoa zao mtu
anapokuchekea haimaanishi anakutaka au anastahili kusumbuliwa mtu
anapokuheshimu na yeye mheshimu.
No comments:
Post a Comment