Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akizindua
Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua leo
jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya
Vitabu na Midahalo (KVM) Bi. Deborah Charles, Agusto Matefu, Mwenyekiti
wa Kamati ya Mijadala na Kongamano ambaye pia ni Mwandishi wa kitabu
hicho Amos Siyantemi na wa mwisho kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Kampeni
ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Kampeni hiyo
inalengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada
zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Amosi Siyantemi
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi
wa Kitabu cha Majipu ya Nchi yetu “ Tushirikiane kuyatumbua leo jijini
Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula
na kushoto Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini
(KVM) Bw. Daniel Zenda.
Waandishi
wa habari wakifuatilia uzinduzi wa Kitabu cha Majipu ya Nchi Yetu
“Tushirikiane kuyatumbua” leo jijini jijini Dar es Salaam. Kitabu hiko
kimezinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula (hayupo
pichani).Uzinduzi wa Kitabu hicho umeenda sambamba na utambulisho wa
Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM). Kampeni hiyo ina lengo la
kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika jitihada zake za
kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akionyesha
Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua mara
baada ya kukizindua leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) ambaye pia
ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na kushoto ni Mratibu wa
Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda.
Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli
katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa
majipu.
Picha zote na: Frank Shija, MAELEZO
No comments:
Post a Comment