Kamati ya Olimpiki
ya Kimataifa imetangaza hatua mpya zitakazolenga kuondoa udanganyifu wa
matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni katika michuano ya Olimpiki
mjiji Rio de Janeiro.
Kamati hiyo imesema kuwa itaongeza bajeti ya vipimo hususan kwa wanariadha kutoka Urusi, Kenya na Mexico.Nchi hizi tatu zimekuwa chini ya viwango vilivyowekwa na shirika la kupambana na dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
Kamati hiyo pia imeahidi kuendelea na upelelezi wa sampuli za awali katika michuano ya Beijing na London.
Mpaka sasa zaidi ya wanaridaha 50 wanatuhumiwa kwa matumizi ya dawa hizo huku 22 wakitokea Urusi.Maamuzi ya iwapo wanariadha wa Urusi watashiriki michuano ya Rio mwaka huu yatatolewa baadae mwezi huu.
No comments:
Post a Comment