Meneja
Mauzo wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka akizungumza na
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Michuano ya Copa America
katika viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki. Copa America imeanza Juni 4 mpaka Juni 26 mwaka huu ambapo
inachezeka nchini Marekani na kushirikisha mataifa 16 ya Marekani ya
Kusini na Kaskazini na kuonekana kupitia chaneli za Sports Focus na Worl
Football.
Wateja
wakinunua ving’amuzi vya StarTimes kwa bei ya shilingi 22,000/-
vilivyounganishwa na ofa ya kifurushi cha Mambo chenye chaneli za Sports
Focus na World Football ili kujionea michuano ya Copa America moja kwa
moja. Copa America imeanza Juni 4 mpaka Juni 26 mwaka huu ambapo
inachezeka nchini Marekani na kushirikisha mataifa 16 ya Marekani ya
Kusini na Kaskazini na kuonekana kupitia chaneli za Sports Focus na Worl
Football.
Hapa wakipiga mpira.
Wateja
wa StarTimes wakiwa na zawadi zao walizojishindia baada ya kununua
ving’amuzi ili kujionea michuano ya kombe la Copa America. Copa America
imeanza Juni 4 mpaka Juni 26 mwaka huu ambapo inachezeka nchini Marekani
na kushirikisha mataifa 16 ya Marekani ya Kusini na Kaskazini na
kuonekana kupitia chaneli za Sports Focus na Worl Football.
Na Tabu Mullah
Mashabiki
wa soka nchini kote wameanza kufurahia mechi za michuano ya kombe la
Copa America ambayo inaonekana moja kwa moja kupitia ving’amuzi vya
StarTimes kwenye chaneli zake za michezo za Sports Focus na World
Football kuanzia Juni 4 mpaka Juni 26 mwaka huu inayopigwa nchini
Marekani.
Akizungumza
katika uzinduzi wa kuanza rasmi kwa michuanoo hiyo katika viwanja vya
Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii Meneja wa
Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka amebainisha kuwa Copa
America imekwishaanza na tayari timu za Marekani na Colombi zimekwisha
fungua pazia.
“Leo
ninayo furaha kubwa kuwafahamisha wateja wetu na watanzania wapenda
soka kwamba michuano ya Copa America inaonekana moja kwa moja kwenye
ving’amuzi vyao vya StarTimes.
Mechi zote za kombe hili 32
zitakazozikutanisha timu kutoka mataifa 16 kwenye viwanja 10 tofauti
nchini Marekani zitaonekana kupitia chaneli zetu za michezo za Sports
Focus na World Football. Anachotakiwa mteja ni kujiunga na malipo ya
mwisho wa mwezi ya kuanzia shilingi 12,000/- na kuendelea na wasio na
ving’amuzi vyetu watembelee viwanjani hapa au maduka, mawakala na ofisi
zetu ili kununua kwa bei nafuu kabisa ya shilingi 22,000/- tu ikiwa na
ofa ya kifurushi cha Mambo kwa mwezi mmoja.” Alisema Bw. Kisaka
Meneja
huyo wa Mauzo alifafanua zaidi kuwa kutokana na tofauti ya muda baina
yetu na nchi ya Marekani ambako michuano hiyo inafanyikia kwa mara ya
kwanza tangu kuanza kwake miaka 100 iliyopita mechi hizo zitakuwa
zikirudiwa kupitia chaneli hizo hizo kuanzia saa saba mchana.
“Kuna
tofauti kubwa kati ya muda na hivyo kusababisha mechi nyingi kuanza
usiku au alfajiri, mechi za mapema kabisa kwa muda wa kwetu zinaanza saa
sita ya usiku. Kwa kulitambua hilo mechi hizo zitakuwa zikirudiwa
mchana ili kila mtu aweze kushuhudia ni kitu gani kinaendelea. Na mpaka
sasa tayari wenyeji Marekani wamekwisha fungua pazia kwa mechi yao ya
kwanza ambayo wamepoteza kwa kufungwa magoli 2 – 0 dhidi ya Colombia.
Msisimko ni mkubwa wa michuano hii kwani wachezaji nyota wote wa dunia
kutoka bara la Amerika ya Kusini watakuwa uwanjani kuhakikisha kombe
linarudi nyumbani. Wachezaji kama Lionel Messi, Luis Suarez, Kun Aguero,
Gonzalo Higuan, Angel Di Maria, Edinson Cavani, James Rodriguez,
Countinho na wengineo wengi.”
Bw.
Kisaka alimalizia kwa kusema kuwa, “Ninapenda kuchukua fursa hii
kuwasihi watanzania kulipia ving’amuzi vyao na kujiunga nasi. Falsafa ya
StarTimes Tanzania ni kutaka kila mtanzania afurahie matangazo ya
dijitali akiwa nyumbani kwake kwa bei nafuu na ndio maana gharama zetu
ni nafuu. Dhamira yetu ni kuwapatia wateja huduma bora zenye uhakika.
Tunafahamu watanzania wanapenda michezo hususani soka na tunajitahidi
kila siku kuwaletea michezo mizuri zaidi kama safari hii Copa America,
awali tumeonyesha ligi za Bundesliga na Seriea A pamoja na kombe la
vilabu bingwa duniani (ICC). Hivyo basi tunawaomba wateja wetu
waichangamkie hii fursa kwa kufurahia kile wakipendacho na StarTimes.”
Michuano
ya Copa America ilianza mnamo mwaka 1916 na mwaka huu inatimiza miaka
100 tangu kuanzishwa kwake. Kwa mafanikio hayo waandaaji wameamua
shamrashamra zake kufanyika nje ya ardhi ya bara la Amerika Kusini,
yaani Marekani. Timu ya taifa ya Uruguay ndiyo inashikilia rekodi ya
kutwaa ubingwa huo mara nyingi zaidi, mara 15 ikifuatiwa na Argentina
mara 14 ambapo mara mwisho walichukua mwaka 1993, na kushika nafasi ya
pili mara tatu mfululizo, safari hii tena wakiongozwa na mchezaji wao
bora wa dunia mara tano, Lioneli Messi mastaa kibao, wanapewa nafasi
kubwa zaidi ya kuibuka mabingwa.
No comments:
Post a Comment