Tuesday, 21 June 2016

Clinton amshinda Trump kwa fedha za kampeni

 
Mgombea wa urais nchini Marekani kupitia tiketi ya chama cha Democrats Hillary Clinton ameweza kuchangisha fedha nyingi za kufanyia kampeni ikilinganishwa na mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump, takwimu zinaonyesha.

Kundi la kampeni ya Bi Clinton lilianza kutafuta fedha mwezi Juni likiwa na dola milioni 42 katika benki huku lile linaloongozwa na Donald Trump likiwa na dola milioni 1.3 pekee.
Mfanyibiashara huyo amedai kwamba amekuwa akifadhili kampeni yake akionyesha kwamba yeye hapiganii maslahi.
Tangu kupewa uteuzi wa chama hicho,uchangishaji wa fedha za kampeni umeimarika.
Kundi lake limetaka kuondoa wasiwasi wowote kuhusu fedha za kampnei likisema pesa zinaingia.
Lakini ufichuzi huo wa hivi karibuni unaonyesha kuwa kamati ya kitaifa ya chama cha Republican ilianza kuchangisha fedha hizo mwezi Juni ikiwa na doma milioni 20 katika benki.
Tofauti ni kwamba miaka minne iliopita ,wakati Mitt Romney alipowania urais ,takwimu hizo zilikuwa dola ilioni 60.
Mnamo mwezi Mei,wafadhili waliipatia kampeni ya bw Trump takriban dola milioni 3.
Bw Trump baadaye aliwakopesha dola milioni 2.2 na hivyobasi kufanya jumla ya fedha zake alizokopa kuwa dola milioni 46.

No comments:

Post a Comment