Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza
Meneja wa wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Iringa Eng.
Daniel Kindole wakati wa ukaguzi wa barabara ya Dodoma –Iringa KM 260
ambapo ujenzi wake umekamilika kwa kiwango cha lami.
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza akitoa taarifa ya hali ya
Miundombinu kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa wakati wa ziara ya waziri huyo katika mkoani Iringa.
Waziri
Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mkoani Iringa. Kulia ni Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi na Kushoto Mkuu wa mkoa wa
Iringa Bi Amina Masenza.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akifafanua
jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa mara baada ya kuanza ziara ya siku nne mkoani Iringa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wakazi wa mikoa ya Dodoma
na Iringa kutumia fursa ya kukamilika kwa kiwango cha lami barabara ya
Dodoma Iringa kufanya shughuli za uzalishaji ili kujiletea maendeleo.
Akizungumza wakati akikagua
barabara ya Dodoma Iringa KM 260 Profesa Mbarawa amesema Barabara hiyo
imelenga kufufua uchumi wa mikoa ya Iringa na Dodoma hususani hifadhi ya
Ruaha na Vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Iringa.
“Barabara hii tuIiigawa katika
sehemu tatu Iringa-Migori KM 95.2, Migori- Fufu KM 93.8 na Fufu –Dodoma
Km 70,9 ili ikamilike kwa haraka na hivyo kuharakisha maendeleo ya watu
wa Dodoma na Iringa “. Amesema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa amesema kiasi cha
sh. bil 4.6 itatolewa na Serikali ili kulipa fidia kwa wananchi
watakaopisha ujenzi wa barabara ya Iringa mchepuo KM 7.3 itakayoanzia
Kihesa –Kilolo kupitia Chuo Kikuu cha Iringa hadi Igumbilo ili kuondoa
msongamano wa magari katikati ya Mji wa Iringa.
Waziri Mbarawa amesisitiza nia ya
Serikali ya kuukarabati uwanja wa Ndege wa Nduli mkoani Iringa ili
kuwawezesha watalii wanaokwenda katika hifadhi ya Ruaha na Vivutio
vingine vya Utalii Mkoani Iringa kutumia uwanja huo ili kuhamasisha
uchumi wa mkoa wa Iringa.
Naye Mbunge wa Isimani Mhe.
Wiliam Lukuvi ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
akizungumza kwa niaba ya wabunge wa Mkoa wa Iringa amemshukuru Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Mbarawa kwa kukubali kujenga
barabara ya Mchepuo ya Iringa na kumuomba aangalie uwezekano wa kujenga
kwa kiwango cha lami barabara ya Iringa-Kalenga hadi katika hifadhi ya
Taifa Ruaha yenye urefu wa KM 104.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina
Masenza amemuomba Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupanua
barabara ya TANZAM eneo la Mlima kitonga na kumalizia ujenzi wa barabara
ya Tosamaganga –Ugwachanya kwa kiwango cha lami na Ujenzi wa daraja la
Tosamaganga ili kupunguza changamoto za usafiri kwa wakazi wa Iringa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano yupo katika Ziara ya siku nne mkoani Iringa kukagua
maendeleo ya Ujenzi wa Miundombinu mkoani humo.
No comments:
Post a Comment