Mgeni Rasmi kwenye hafla ya
uzinduzi wa Bodi ya tano (5) ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene (Mb) alipokea maelezo ya utangulizi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Prof. Faustine Karani Bee na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo. Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqarro.
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini
iliyozinduliwa pamoja na Menejimenti ya Mfuko wa LAPF wakisilikiza kwa
makini hotuba ya uzinduzi wa Bodi toka kwa Mgeni Rasmi Mh. George Simbachawene, Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (TAMISEMI).
Mwenyekiti wa Bodi ya tano (5)
ya Wadhamini Prof. Faustine Karani Bee akitoa maelezo ya msingi kuhusu
Mfuko wa LAPF mbele ya Mgeni Rasmi kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini
wa Mfuko tarehe 04 Februari, 2017.
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais
(TAMISEMI) Mh. George Simbachawene (Mb). akitoa hotuba ya uzinduzi wa
Bodi mpya ya Mfuko wa LAPF mbele ya Mwenyekiti wa Bodi, Wajumbe wa Bodi,
Menejimenti ya Mfuko na wanahabari, tarehe 04 Februari, 2017.
Mmoja wa Wajumbe wapya wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Ndg. Tumaini P. Nyamuhokya akijitambulisha mbele ya Mgeni Rasmi wakati wa uzinduzi wa Bodi ya tano (5) ya Mfuko wa LAPF.
Mgeni Rasmi kwenye uzinduzi wa
Bodi ya tano (5) ya mfuko wa LAPF Waziri wan chi – Ofisi ya Rais
(TAMISEMI) Mh. George Simbachawene (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh.
Gabriel Daqarro, Mwenyekiti wa Bodi Prof. Faustine Bee, Wajumbe wa Bodi
pamoja na Menejimenti ya Mfuko mara tu baada ya uzinduzi wa Bodi.
No comments:
Post a Comment