Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi askari 12
waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya wakati uchunguzi
ukiendelea.
IGP huyo amewaambia wanahabari, Jumamosi ya leo tarehe 04-02-2017 katika makao makuu ya
Polisi huku akisema kuwa Polisi ndiyo chombo kinachoongoza mapambano juu
ya madawa hayo, huku akisema kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya askari
atakayetuhumiwa.“Tumeamua kuwasimamisha kazi wote walioguswa moja kwa moja na sakata hili, pia Polisi itachukua hatua madhubuti ikiwemo kuwapeleka mahakamani wasanii waliotuhumiwa,” alisema.
Askari hao ni wale waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda siku mbili zilizopita wakati akiwaambia wanahabari juu ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara na matumizi ya madawa hayo.
No comments:
Post a Comment