Thursday, 30 June 2016

Kagame kufungua Sabasaba leo

  Na Mwamvita Mtanda
 
Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba, yanatarajiwa kufunguliwa leo na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ikiwa ni maonesho ya kwanza ya mpango wa pili wa miaka mitano ya ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 1 2016


Misikiti na makanisa yafungwa Lagos Nigeria

 
Mamlaka katika mji wa Lagos nchini Nigeria umefunga makanisa 60 na misikiti 20 katika jitihada za kupunguza kelele.

Zlatan Ibrahimovic akaribia kutua Man Utd

 Ibra
Mshambuliaji nyota kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovicn anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake kujiunga an Manchester United wiki hii.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 34, kwa sasa hana mkataba na klabu yoyote baada yake kuondoka Paris St-Germain.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu amefikishwa mahakamani leo

 
  Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu akifika  katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam mchana huu. Ikiwa jana Mbunge huyo alihojiwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Polisi cha Kanda maalumu ya Dar es Salaam na kutupwa Rumande mara baada ya kukosa dhamana.

Serengeti Boys imeondoka leo kwenda Shelisheli kwa ajili ya kuwavaa wenyeji katika mchezo wa marudiano


 
Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeondoka saa 9.45 alfajiri ya leo Juni 30, 2016 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia kwenda Visiwa va Hame-Shelisheli kwa ajili ya kuwavaa wenyeji katika mchezo wa marudiano kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana.

Mwandishi wa ''The Concubine'' afariki

Elechi Amadi

Mwandishi maarufu wa Nigeria Elechi Amadi amefariki akiwa na umri wa miaka 82.
Amadi ambaye aliandika vitabu maarufu kama vile The Concubine,Isiburu,Sunset in Biafra,Peppersoup na The Road to Ibadan alifariki siku ya Jumatano mwendo wa saa tisa,wiki moja baada ya kuripotiwa kuugua.

Ukawa wavaa nguo nyeusi, wabeba mabango ya ujumbe kwa JPM, Dkt. Tulia









WABUNGE wa Kambi Rasmi ya Upinzani leo asubuhi wameingia bungeni wakiwa wamevalia nguo nyeusi wote walipohudhuria kikao cha 54 cha Bunge la Bajeti mjini Dodoma.
Baada ya Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson kuingia bungeni na kuongoza dua ya kuliombea Bunge, walianza kunyanyua mabango yenye ujumbe mbalimbali huku wakitoka nje ya ukumbi wa bunge hilo.

Wabunge watatu wa Ukawa wasimamishwa kutohudhuria vikao bungeni

  Na Golden Mwakatobe
 
Bunge limeridhia pendekezo la adhabu ya kumsimamisha vikao 10 kuanzia leo Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi baada ya kutiwa hatiani na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kudharau mamlaka ya Spika.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kepten Mstaafu George Mkuchika alisema alinyoosha kidole cha kati kwenda juu cha mkono wa kulia huku vingine akivikunja  jambo ambalo ni matusi na dharau kwa mamlaka ya Bunge.

Vanessa Mdee:Mfumo mfumo wa label za Marekani haufai Afrika



mfumo wa label za Kimarekani hauwezi kuzaa matunda kwenye muziki wa Afrika. Nilimuuliza of course, iwapo anaweza kusainishwa label, na haya ndio yalikuwa majibu yake:
Mfumo wa label Afrika ni tofauti kabisa, the concept of record label ilianzia nje, Marekani, Europe, Australia au nchi nyingine ambazo zinastructure kwenye industry. Sisi bado tunapigania mirabaha. So when you tell me a label inanisaidia, inanisaidia kwa kipi zaidi? Wananipa nini? Labda nasaini distribution deal watanisaidia kusambaza muziki, great, labda wana nguvu za kunishinda mimi peke yangu. Lakini when you think of things the label supposed to do, I don’t know of any label in Africa, sijui.”

Mlipuko wa bomuwaua watu 18 Somalia

 
watu 18 wameuawa baada ya bomu kulipuka na kuharibu kabisa basi walimokuwa wakisafiria katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara lililipua gari lililokuwa limewabeba abiria. Wote waliouawa walikuwa raia.

Fella: Ruby ana ‘stress’ ndio maana hajaonekana kwenye video ya Yamoto Band

 
Na Tabu Mullah
 
Ruby alikuwa ana ‘stress’ ndio maana alishindwa kutokea kwenye video ya wimbo SU wa Yamoto Band alioshirikishwa
Meneja wa kundi hilo, Said Fella amekiambia kipindi cha E News cha EATV kuwa hiyo ndio sababu aliyokuwa akipewa na Ruby. Amedai kuwa baada ya kuona kuwa Ruby amekuwa akitoa sababu hiyo kwa muda na hawakutaka asishiriki akiwa hana mood, walilazimika kuifanya bila yeye.


TP Mazembe kumnyakua mchezaji wa yanga Juma Mahadhi kwa gharma yoyote


 Na Kalonga Kasati
 
Moja ya kauli zilizotolewa na TP Mazembe walivyotua Tanzania kupambana na Yanga, ni kuwea mbali na mechi hiyo pia walipanga kuondoka na wachezaji wenye vipaji kutoka Tanzania kama walivyofanya kwa Mbwana Samatta.

Na baada ya mechi hiyo ya juzi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam na kuibuka na ushindi wa bao 1-0, jina la winga mpyawa Yanga, Juma Mahadhi, ndio lilinasa kwenye akili za mashabiki na mabosi wa Mazembe kama ilivyokuwa kwa Samatta mwaka 2011.

Wednesday, 29 June 2016

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 30 2016

Padri apiga marufuku maharusi kupaka ‘Lipstick’

 

 Na Mwandishi Wetu

Waumini wanawake wanaokwenda kufunga ndoa katika  Kanisa Katoliki Parokia ya Hananasif Kinondoni, jijini Dar es Salaam wamepigwa marufuku kupaka rangi ya mdomo  ‘Lipstick’ wakati wa ibada ya misa takatifu ya ndoa.

Al Ahly kama Yanga, yadundwa kwa mara ya pili CAF

Klabu ya soka ya Al Ahly nayo ipo mashakani kutinga hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kukubali kipigo cha pili mfululizo ambapo jana walifungwa nyumbani mabao mawili kwa moja dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Uingereza yazuiwa kuhudhuria mkutano wa EU

 
Uingereza imezuia kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ulaya ambapo itakuwa mara ya kwanza kufanyiwa hivyo kwa miaka 40.

Mahakama Kuu Arusha Yatengua ushindi wa Mbunge wa Longido, Onesmo Ole Nangole (CHADEMA), yaamuru kurudiwa uchaguzi katika jimbo hilo.

Kesi iliyokuwa inaunguruma kuanzia tarehe 29.02.2016 katika mahakam kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii

Chris Brown agombana na meneja wake

Chris Brown

Msanii wa muziki wa RnB, Chris Brown, amegombana na meneja wake anayejulikana kwa jina la Mike G, kwa kumtuhumu kuiba fedha zake.
Inadaiwa kwamba msanii huyo alipoteza fedha hivi karibuni huku akiwa na meneja huyo.
Hata hivyo, meneja huyo amesema alikuwa na mpango wa kuachana na msanii huyo hivi karibuni lakini kutokana na jambo hilo atasubiri liishe ili aweze kuendelea na mambo yake.


Rais Magufuli Aeleza Sababu ya Kutengua Uteuzi wa Mkuu wa Wilaya Ya Ikungi

 Na Kalonga Kasati

Juni 26 mwaka huu Rais John Pombe Magufuli alitangaza kuteua Wakuu wa Wilaya zote nchini, na Wakuu wa Mkoa watatu. Kati ya Wakuu wa Wilaya 139 walioteuliwa, 39 wamebakishwa katika nafasi zao huku 100 wakiwa ni wapya.
Katika hali ya kushangaza siku moja baada ya orodha hiyo kutangazwa, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa wilaya ya Ikungi iliyopo mkoani Singida. Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Bwana Fikiri Avias Said ndani ya masaa 24 tangu uteuzi wake.

Alichokiandika Rais Magufuli kuhusu ugunduzi wa gesi ya Helium nchini Tanzania


Jana ziliripotiwa taarifa kuwa watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalamu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.

Leo June 29 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kupitia account yake ya twitter amepost akizungumzia ugunduzi huo huku akitoa wito kujipanga katika eneo la mikataba.

"Tunamshukuru Mungu Tanzania tumegundua gesi aina ya Helium(He),wito wangu kwa wachumi,wanasheria na watanzania wote kwa ujumla tujipange

England yapata kocha wa muda

 
Chama cha soka nchini England kinajiandaa kumtangaza Gareth Southgate kuwa kocha wa muda wa timu yake ya taifa katika mwanzo wa kampeni za kuwania kufuzu kombe ka dunia.
Zoezi la kumsaka kocha mpya litaanza baada ya michezo ya awali ya kufuzu kufanyika.

Serena na Murry waingia mzunguko wa pili

 
Serena Williams na Andy Murray wamefanikiwa kutinga katika mzunguko wa pili wa michuano ya Wimbledon inayoendelea mjini London. Kwa upande wa Serena yeye amemchakaza Amra Sadikovic kwa seti 6-2,6-4 huku Murray akimchapa Liam Broady kwa seti 6-2 6-3 6-4 katika mchezo uliokuwa wa kukata na shoka.

Korea Kusini,Japan na Marekani zafanya zoezi la kijeshi

 
Korea Kusini, Marekani na Japan zimefanya zoezi la ushirikiano la kukabiliana na makombora katika maji ya jimbo la Hawaii.

Taarifa ya kupimwa UKIMWI nyumba kwa nyumba yatolewa ufafanuzi


 Na Golden Mwakatobe
 
Baada ya kuwepo na taarifa mbalimbali zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii zinazotokana na habari iliyoandikwa na kuchapishwa kwenye gazeti la Jambo leo la June 24 2016, toleo namba 2482 yenye kichwa cha habari “Sasa ukimwi kupimwa nyumba kwa nyumba

Tuesday, 28 June 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 29 2016

 

Yanga VS TP Mazembe

Watu 25 wauawa Yemen

 
Ripoti kutoka nchini Yemen zinasema kuwa shambuli la angani lililofanywa na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia limesababisha vifo vya watu 25 katika mkoa ulio kusini wa Taiz.
Taarifa zinasema kuwa 15 kati ya wale waliouawa walikuwa ni waasi wa Houthi na wengine ni raia.

Hifadhi kubwa zaidi ya gesi ya Helium yagunduliwa

 Hifadhi kubwa zaidi ya gesi ya Helium yagunduliwa 

Tanzania ni miongoni mwa mataifa chache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.

Aliyeibuka wa kwanza katika mtihani India afungwa jela

 
Mwanafunzi mmoja wa India amehukumiwa kifungo jela kwa kudanganya katika mtihani baada ya kujaribiwa kwa mara ya pili.
Ruby Rai mwenye umri wa miaka 17 ambaye alikuwa wa kwanza katika mtihani huo katika jimbo la Bihar, alisema katika mahojiano kwamba somo alipendelo la sayansi ya siasa linahusu mapishi.
Baada ya kanda hiyo kusambaa ,bi Rai alilazimika kukalia tena mtihani na alikamatwa aliposhindwa huku matokeo yake ya mtihani yakifutiliwa mbali.

Vituo vya mafuta vyapokonywa leseni Kenya

 
Tume ya kudhibiti nishati nchini Kenya (ERC), imevipokonya leseni vituo vya mafuta kwa kuuza mafuta machafu.
Uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa mafuta ya diesel au petroli, yalikuwa yamechanyanga na mafuta taa pamoja na bidhaa zingine.

ALIKIBA na DIAMOND ni Siasa ya Tanzania, Hatuoni Shida Kufanya Nao Kazi Wote – SAUTI SOL

Member wa kundi la Sauti Sol, Savara amesema kufanya kazi na Alikiba haimaanishi kuwa wanamkubali zaidi kuliko Diamond. Kundi hilo lilifanya wimbo Unconditionally Bae na Alikiba uliofanya vizuri. “Mambo ya Alikiba na Diamond hiyo ni siasa ya Tanzania,” member wa kundi hilo,

kikosi cha yanga kitakachovaana na Tp Mazembe ya Congo leo

Mashabiki 40,000 kuwaona Yanga, Mazembe uwanjani

  Na Kalonga Kasati

Dar es Salaam. Mashabiki 40,000 wakiwamo 500 wa TP Mazembe watashuhudia mchezo leo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na TP Mazembe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Uwanja wa Taifa una uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 kwa wakati mmoja, lakini kutokana na uamuzi wa viongozi wa Yanga kuwataka mashabiki kuingia bure CAF imeamua kupunguza idadi ya mashabiki kwa sababu za kiusalama.

Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amejiuzulu

 
Saa chache tu baada ya timu ya kandanda ya Uingereza kubanduliwa nje ya mashindano ya mwaka huu ya Euro 2016, Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amejiuzulu wadhfa wake.
Hodgson alikuwa ameshuhudiwa uingereza ikiambulia kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Iceland katika mkumbo wa 16 bora huko ufransa.

Rais wa Argentina amsihi Messi asijiuzulu

 
Rais wa Argentina Mauricio Macri amemwita nyota wa soka wa nchi hiyo Lionel Messi kwa lengo la kumuomba atengue maamuzi yake ya kujiuzulu kucheza soka la kimataifa.

Wimbo wa matusi wamtia 50 Cent matatani Caribbean

 
Mwanamuziki wa kufoka kutoka Marekani 50Cent alilazimika kulipa faini ya dola elfu ishirini pesa za Marekani baada ya kutumia maneno yenye matusi alipokuwa akiwatumbuiza mashabiki wake huko katika kisiwa cha St Kitts and Nevis.
Fifty cent ambaye anafahamika kwa jina kamili Curtis Jackson alikuwa amepangiwa kuwa 'Mcee' katika tamasha hilo la muziki huko Caribbean lakini alipopanda jukwaani mashabiki walimsihi awape kionjo cha muziki wake.

Tunaitafakari Uingereza bado:Marekani

 
Kufuatia kura ya maoni ya Uingereza kujitoa ndani ya Jumuiya ya Ulaya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekari John Kerry amesema Marekani inaangalia mfumo wa ushirikiano na Uingereza kiuchumi.

Wananchi wanaoishi kandokando ya reli kuondolewa kinguvu

  Na Chrispino Mpinge
 
Wizi wa miundombinu, uchakavu wa reli pamoja na shuguli za kibinadamu zimeonekana kuwa chanzo kikuu cha ajali za Treni hasa katika maeneo mengi ya njia hizo hali inayosababsha hasara kwa serikali ya mabilioni ya fedha kila mwaka kwa ajili ya ukarabati wa reli hizo.

Namna ya kujua kama umeishiwa maji mwilini

 Na Kalonga Kasati

Umeshawahi kwenda hospitali kumlalamikia daktari kuwa mwili wako hauna nguvu na unajisikia kuchokachoka sana na baada ya kukuchunguza, akakwambia huna tatizo lolote isipokuwa una upungufu wa maji mwilini tu?
Mwili kuishiwa nguvu huwa ni miongoni mwa dalili za upungufu wa maji mwilini na chanzo kikiwa ni wewe mwenyewe kutopenda kunywa maji. Ni kawaida kwa baadhi ya watu kutokunywa maji hadi pale wanaposikia kiu.