Tuesday, 28 February 2017

ZILIZOSHIKA HATAMU KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MAR 01 2017

 

kuvunja rekodi ya usaji wa Paul Pogba

Manchester United wana pesa,ni kati ya timu ambazo zikikamia kukuchukua zitakuchukua tu.Dunia haikuamini kiasi United walichokitoa kumrudisha Paul Pogba Old Trafford.Dau la £89m lilizitoa hata Barcelona na Madrid katika mbio za kumtaka Pogba.Lakini kocha wake Jose Mourinho anaamini siku sio nyingi Pogba anaweza azidiwe dau la usajilu na mchezaji mwingine.Hawa wafuatao kwa wanachokifanya sasa na hali zao klabuni wanaweza kuvunja rekodi ya usajili wa Pogba.
Antoine Griezman(Athletico Madrid).Anaweza kufikia hata thamani ya £100m kwa sasa.Ni mchezaji watatu kwa ubora duniani akiwa nyuma ya Messi na Ronaldo,Griezman ameanza kuhusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United,ameshawahi kukiri ugumu wa yeye kuhamia katika vilabu vya Hispania (Madrid na Barcelona).Lakini pesa za miamba hiyo miwili zinaweza kuvunja rekodi ya usajili aliyonayo Pogba kwa sasa.Kuwepo katika tatu bora ya Ballon D’or na mchezaji bora wa FIFA sio kitu kidogo na kinaweza kulifanya dau lake la usajili likawa kubwa kuliko la Pogba.
Neymar Jr(Barcelona).Tafiti mbali mbali zimemtaja Neymar kama mchezaji ambaye thamani yake ndani na nje ya uwanja,ni wazi kwamba Neymar hawezi kung’ara sana akicheza pembeni ya Messi,yupo katika timu ambayo nafasi ya ushambuliaji kuna wafalme wengine.Ili Neymar awe mkubwa zaidi ni lazima awe katika timu ambayo ataonekana mkubwa.Anahusishwa na kuuzwa timu mbalimbali ikwemo PSG na United hawachezi mbali.Lakini unadhani uhamisho wa Neymar utakuwa wa kitoto?laa hasha Neymar ni lazima atasajiliwa kwa rekodi itakayoishtua Dunia.

TFDA Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Uvumi Wa Dawa Aina Ya P-500 (Paracetamol)



Serikali imesema itaendelea kuwajengea uwezo wanawake ili kuweza kushiriki katika shughuli za matengenezo na ukarabati wa miundombinu ya barabara

1
Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Mwanza (Tanroads) Eng. Marwa Rubirya (wa pili kushoto) akizungumza na wawakilishi wa vikundi vya wanawake wanaoshiriki mafunzo ya ukarabati na matengenezo ya barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi, Jijini Mwanza.
2
Mratibu Kitengo cha ushirikishaji wa wanawake katika kazi za barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) Eng. Rehema Myeya (wa pili kulia) akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo ya ukarabati na matengenezo ya barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi, Jijini Mwanza kushoto ni Eng. Liberata Alphonce kutoka sekta ya ujenzi na wapili kushoto ni Meneja wa Tanroads mkoa wa Mwanza Eng. Marwa Rubirya.
3
Eng. Liberata Alphonce kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sekta ya (Ujenzi) wa pili kulia akitoa maelezo kwa washiriki wa mafunzo ya ukarabati na matengenezo ya barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi, Jijini Mwanza.
4
Mkufunzi wa mafunzo ya kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi kutoka Chuo cha Teknolojia stahiki ya nguvu kazi Mbeya (ATTI) Eng. Richard Kansimba akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo ya ukarabati na matengenezo ya barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi, Jijini Mwanza.
5
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya ukarabati na matengenezo ya barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi akichangia mada juu ya teknolojia hiyo.
6
Washiriki wa mafunzo ya ukarabati na matengenezo ya barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi wakifuatilia mada hiyo Jijini Mwanza.

Serikali imesema itaendelea kuwajengea uwezo wanawake ili kuweza kushiriki katika shughuli za matengenezo na ukarabati wa  miundombinu ya barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Mwanza (Tanroads) Eng. Marwa  Rubirya wakati akifungua mafunzo ya kozi kwa wanawake wa vikundi vya mikoa ya Kanda ya ziwa jijini Mwanza.
“Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sekta ya (Ujenzi) imekuwa ikitekekeza sera mbalimbali ikiwemo shughuli za matengenezo yenye kuongeza ushiriki wa wanawake katika kazi za barabara ili waweze kujikwamua kiuchumi”. amesema Eng.Rubirya.
Eng. Rubirya amewataka  wanawake kusijili vikundi vyao kupitia bodi ya usajilibwa Makandarasi nchini (CRB)  ili zabuni za kazi za ukaraba na matengenezo ya barabara zinapotangazwa waweze kukidhi vigezo vya kupata kazi hizo.
Aidha, Eng. Rubirya amewahimiza wakinamama hao kufanya kazi hizo kwa ubora unaotakiwa pindi wapatapo kazi hizo ili barabara hizo ziweze kudumu kwa muda mrefu na kuleta faida kwa wananchi.
Naye  muwezeshaji katika mafunzo hayo Eng. Liberata Alphonce amesema Serikali imelenga kuinua uchumi wa wanawake wenye nia ya kufanya kazi za barabara  kwa vile uchumi wa mwanamke ukiimarika na taifa pia litaimarika.
“Kwa muda mrefu kazi za barabara zimekuwa zikionekana za kiume sasa umefika wakati wa wanawake kushiriki katika kazi hizo kwa vile uwezo tunao.” amesisitiza Eng.Alphonce.
Kwa upande wake Mratibu wa kitengo cha ushirikishaji wanawake katika kazi za barabara Eng. Rehema Myeya amesema Wizara imeona umuhimu wa kutoa mafunzo yatakayowasaidia wanawake kuwa na uwezo wa kufanya kazi za ukandarasi hasa wa barabara hususan matengenezo na ukarabati.

Jinsi ya kuandika barua ya kuomba kazi


Je ulishawahi kuandika barua ya maombi ya kazi na kutuma kwa waajiri wengi na wote au wengi ya hao hawakukujibu hata kama unajua unazo sifa za hiyo kazi?

Jibu la hapo ni rahisi

hapo Uandishi wa barua zako una shida tu..


Barua ya maombi ya kazi iwe na sura hii

  1. Wewe nani
  2. Umezipataje hizo taarifa za nafasi za kazi
  3. Unafikiri wewe utapeleka kitu gani nzuri ambayo wengine walioomba hiyo nafasi hawana ila wewe unayo/unazo (Usieleze habari za degree, diploma au vyeti vyako kwani na wenzako wanazo, pia usieleze juu ya uzoefu wako wa kazi kwani na wao wanazo tena kukuzidi)
  4. Eleza utayari wako wa usaili na kuanza kazi
  5. Acha mawasiliano yako ya haraka kama simu ya kiganjani na barua pepe (usiache mawasiliano ya kupitia kwa watu wengine kama shangazi mjomba, mama, baba na marafiki au jirani)
  6. Eleza kwamba umeambatanisha wasifu wako

Bosou kuondoka Yanga

Hali inaonekana kuwa si shwari kihivyo ndani ya klabu ya Yanga, hasa baada ya mashabiki wa klabu hiyo kumshambulia beki Vincent Bossou mtandaoni.
Mashabiki wa Yanga wanaonyesha kuchukizwa na Bossou kutokana na uamuzi wake wa kutotaka kucheza katika kikosi hicho.
Taarifa zinaeleza Bossou amegoma kucheza kwa kuwa anadai mshahara wake wa miezi kadhaa.
Lakini kupitia mtandao wa Instagram, Bossou amesema anaidai Yanga mshahara wa miezi minne.
Ingawa Bossou Kingereza chake ni cha "kuunga" amewajibu mashabiki wa Yanga, kwamba yuko tayari kuondoka ila wamlipe mshahara wake wa miezi minne.

Watalii wawili kusafirishwa kwenda mwezini 2018

Roketi itakayotumika kuwasafirisha watalii hao
  Kampuni ya kibinafsi ya kurusha roketi imetangaza kwamba watalii wawili wamelipa kupelekwa mwezini.
Safari hiyo itafanyika 2018 kulingana na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SpaceX Elon Musk, alieongezea kwamba watalii hao tayari wamelipa kiasi fulani cha fedha.
''Hatua hiyo inatoa fursa kwa binaadamu kurudi katika anga za juu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 45'',alisema.
Wawili hao ambao majina yao hayakutajwa wataelekea mwezini wakiwa katika meli hiyo ya angani ambayo itafanyiwa jaribio lake la kwanza la kurusha rekoti isiokuwa na rubani.
Bwana Musk alisema kuwa ushirikiano wa shirika la sayansi na teknolojia ya angani nchini Marekani Nasa umefanya ufanisi wa safari hiyo.

Watalii wawili kwenda mwezini 2018
Amesema kuwa abiria hao wawili watasafirishwa kwa kasi zaidi ya watu wengine wowote kuwahi kusafirishwa katika sayari.
Bwana Musk hatahivyo amekataa kuwataja abiria hao wawili ,akisema kwamba ni watu wanaojuana na kwamba hawatoki Hollywood.


Mmiliki wa Samsung afikishwa mahakamani kwa kutoa hongo



Mrithi wa kampuni tajiri zaidi nchini Korea Kusini, Samsung, atafikishwa mahakamani kwa madai ya kutoa hongo na ubadhirifu wa pesa, katika sakata kubwa inayoendelea kutokota, ambayo pia imesababisha kutimuliwa kwa rais, Park Guen-hye.
Mwendesha mashtaka maalum amesema kwamba, Lee Jay-yong, pamoja na wakuu wengine wanne wa Samsung watashtakiwa.

Bwana Lee, aliyekamatwa mapema mwezi huu, anashtakiwa kwa madai ya kutoa hongo ya takriban dola milioni 40, kwa mshirika wa karibu wa rais wa zamani, ili kupata usaidizi wa kisiasa.

Leicester City yaichapa Liverpool


Klabu ya soka ya Leicester City imefanikiwa kupanda hadi nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga Liverpool kwa mabao 3-1 usiku wa Jumatatu hii.
Magoli ya mabingwa hao watetezi wa kombe hilo yalifungwa na Jamie Vard aliyefunga magoli mawili kwenye dakika ya 28 na 60, Danny Drinkwater dakika ya 68 na goli la kufutia machozi la Liver lilifungwa na Philippe Coutinho dakika ya 68.
Huo umekuwa ni mchezo wa kwanza wa Leicester kushinda wakiwa chini ya kocha wao mpya wa muda Craig Shakespeare ambaye amekalia kiti hicho baadaya Claudio Ranieri kutimuliwa wiki iliyopita.
Liverpool ambao wanashika nafasi ya tano kwenye ligi kuu walikuwa na nafasi kubwa ya kupanda hadi kwenye nafasi ya tatu iwapo wangeweza kushinda mechi hiyo.

Monday, 27 February 2017

MGAZETI YA LEO FEB 28 2017 JUMANNE

 

Mhe Job Ndugai amewaahidi Viongozi wa Chama cha Skauti Tanzania ushirikiano katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali

1
Spika wa Bunge  Mhe Job Ndugai akizungumza na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Skauti waliomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam mapema leo. Wa pili  kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Eng. Stella Manyanya (Mb) na anayefutia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Skauti Tanzania Balozi Nicholas Kuhanga.
2
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Eng. Stella Manyanya (Mb) aliyeambatana na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Skauti Tanzania akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati walipotembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
3
Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Skauti Tanzania Balozi Nicholas Kuhanga akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
4
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (aliyekaa kulia) na  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Eng. Stella Manyanya (Mb) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Skauti Tanzania mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Picha na Ofisi ya Bunge
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   Mhe Job Ndugai amewaahidi Viongozi wa Chama cha Skauti Tanzania ushirikiano katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama hicho ikiwemo maadhimisho ya Siku ya Skauti Afrika na Maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini.
Mhe Spika aliyasema hayo wakati alipokutana na kuzungumza na  Viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Skauti Tanzania  Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam ambao walimuomba awaunge mkono katika shughuli zao.
Spika Ndugai aliwaeleza Viongozi hao kwamba kwa niaba ya Wabunge wote ameupokea ujumbe huo na atajitahidi sana katika kuhufikisha kwa Waheshimiwa Wabunge.
“Ninawashukuru sana kwa ujumbe huu na niwaahidi kwamba tupo pamoja si katika hili tu bali katika mambo yoyote ambayo mtakuwa mkiyafanya na nawaahidi pia ushiriki wa Waheshimiwa Wabunge katika maadhimkisho hayo,” alisema Mhe Spika.
Awali akimuelezea Mhe Spika kuhusiana na Shughuli mbalimbali za Skauti hapa nchini Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Stella Manyanya ambaye aliambatana na Viongozi hao wa Skauti alisema pamoja na majukumu mengine Chama hicho cha Skauti kina kazi kubwa ya kuandaa maadhimisho ya Siku ya Skauti Dunia na Maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini.
Mhe Manyanya alisema   kuwa maandalizi ya  Maadhimisho ya siku Skauti Afrika ambayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 8 hadi 11 Machi mwaka huu mkoani Arusha yanaendelea vizuri ingawa kuna changamoto kubwa ya kifedha katika maandalizi ya maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini ambayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Juni hadi Julai Mkoani Dodoma.
“Mhe Spika kumekuwa na jitihada mbalimbali za kufanikisha maadhimisho haya lakini kumekuwa na changamoto katika kufikia malengo na ndio maana tumefikana hapa ili kukuomba utuunge mkono” alisema Mhe Manyanya.

(TPSF) imetoa wito kwa wahitimu na vijana waliopo vyuoni kuchangamkia fursa ya mpango maalum

Godfrey-Simbeye
Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) imetoa wito kwa wahitimu na vijana waliopo vyuoni kuchangamkia fursa ya mpango maalum uliobuniwa baina yake na Serikali ambao umekusudia kuwajengea ujuzi kabla ya kuajiriwa  ili waweze kufanya kazi kwa weledi.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye wakati alipokuwa akichangia mada kuhusu wahitimu wa vyuo vikuu kushindwa kuonyesha ujuzi baada ya kuajiriwa.
“Upo upungufu mkubwa wa mafunzo ya vitendo kwa wahitimu wengi wanaomaliza vyuo vikuu nchini na imedhihirika kuwa wahitimu hao hushindwa  kufanya kazi kwa weledi wanapokuwa wameajiriwa na sekta mbali mbali.
Alisema kuwa mpango huo maalum umeanzishwa kwa lengo la kuwatayarisha  wahitimu wa vyuo kupata mafunzo ya muda mfupi ili kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo pindi wanapoajiriwa au kutaka kujiajiri.
Simbeye alisema Mpango huo pia umekusudia kuwapunguzia gharama waajiri, hasa wa sekta binafsi kwa kuwa wengi wao wamekuwa wakitumia pesa nyingi kwa kuwapeleka waajiriwa wapya katika mafunzo ili waweze kumudu kazi zao.
Akifafanua zaidi alisema katika mpango huo waajiriwa wataweza kupata mafunzo mtambuka na  gharama zote za mafunzo zinagharimiwa na Serikali.
“Chini ya mpango huu, wahitimu na vijana walioko vyuoni wanatakiwa kujiandikisha kwa hiari, na baada ya mafunzo inakuwa rahisi kwao kupata ajira kupitia katika sekta binafsi au makampuni” aliongeza Bwana Simbeye.

Uongozi wa klabu ya Yanga, umewaomba radhi mashabiki na wanachama

Uongozi wa klabu ya Yanga, umewaomba radhi mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kwa matokeo mabaya waliyoyapata juzi Jumamosi dhidi ya Simba.
Katika mchezo huo Yanga ilifungwa bao 2-1 na Simba mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amewaomba radhi mashabiki, wanachama na wapenzi wa timu hiyo kuendelea na utulivu wao katika kipindi hiki ambacho wamepoteza mechi muhimu.
“Matokeo haya tuliyopata ni ya kimchezo, kikubwa ni kupambana na michezo iliyobaki mbele yetu na kuendelea kuwapa ushirikiano wachezaji kwani bado tuna mashindano mengi na michezo mingi mbele yetu, tunaamini kocha ameona mapungufu kwenye mchezo uliopita na atayafanyia kazi na kurejesha furaha yetu,” inasema taarifa hiyo ya Mkwasa.

Meneja mradi wa Quality Group na katibu wamefikishwa katika Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kukiuka amri ya afisa uhamiaji,


Meneja mradi wa Quality Group na katibu wake Leo mapema wamefikishwa katika Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kukiuka amri ya afisa uhamiaji, na kujaribu kutoroka.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu hiyo, Cpyrian Mkeha.
Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Uhamiaji, Method Kagoma aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Jose Kiran Meneja Mradi na Prakash Bhatt.
Akisoma hati ya mashtaka Kagoma amedai kuwa Februari 20, mwaka huu, washtakiwa hao wakiwa raia wa India na waajiriwa wa Quality Group Ltd, walimzuia afisa wa Uhamiaji kufanya kazi zake.
Kagoma amedai kuwa, watuhumiwa hao walikataa kuripoti katika ofisi za Uhamiaji zilizopo jijini Dar Es Salaam kwa kujaribu kutoroka nchini Tanzania kwa kupitia mpaka wa Horohoro,ambao ni mpakani mwa Tanga na Mombasa,nchini Kenya.

, Dkt. Khamis Kigwangalla amehairisha press conference ya kutangaza majina ya mashoga wanaojiuza na kujitangaza mitandaoni.

Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangalla, amesema kuwa hawatokuwa na press conference ya kutangaza majina ya mashoga wanaojiuza na kujitangaza mitandaoni.
Waziri huyo aliahidi kutangaza majina na mashoga ambao wanatuhumiwa kujiuza mtandaoni kinyume na sheria.

Jumatatu hii waziri huyo alitoa taarifa ya kuahirisha kutaja majina hayo kwa madai kuna matatizo ya kiufundi.
“Tunaomba radhi hatutokuwa na press conference kuhusu kutangaza majina ya mashoga wanaojiuza mitandaoni kwa sababu za kiufundi!,” alitweet Kingwangala.
Hata hivyo hakuweka wazi kama itafanyika tena.


Habari katika Picha

1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba  akiwa katika kikao  na wawakilishi wa sekta binafsi wakizungumza kuhusu masuala ya ufanisi katika mchakato wa Tathmini ya athari za Mazingira. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustin Kamuzora. Kikao hiko kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.
2
Baadhi ya Wadau wa sekta binafsi waliohudhuria kikao hiko wakiwa pamoja na Watumishi na Wataalamu toka Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Usimamizi wa mazingira(NEMC) wakimsikiliza Mh. Waziri January Mkamba(hayupo pichani) wakati wa kikao hiko.
3
Mmoja wa Wadau toka sekta binafsi za wenye mahoteli, viwanda na fukwe Bi. Lathifa K. Sukes akichangia jambo katika kikao hiko. (PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI OMR)

Muwekezaji aliidanganya serikali pamoja na kumdanganya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda

Waziri William Lukuvi
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema itamchukulia hatua muwekezaji aliyetoa ardhi kwa serikali ya mkoa wa dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, kwa madai kuwa ardhi aliyoitoa siyo yake.
Waziri wa wizara hiyo, William Lukuvi, ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam na kufafanua kuwa muwekezaji huyo aliidanganya serikali pamoja na kumdanganya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ambaye ndiye aliyekabidhiwa eneo hilo kwa niaba ya serikali.
Mbali na kosa la kuidanganya serikali, Lukuvi pia amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara huyo kwa kumiliki ardhi kinyume cha sheria.
Kuhusu Mkuu wa Mkoa , Paul Makonda, Lukuvi amesema tayari amekwishafanya naye mawasiliano na kumuelewesha kuwa alidanganywa kwa kuambiwa kuwa anapewa eneo kwa ajili ya viwanda, huku eneo lenyewe likiwa ni mali ya serikali.


Siku ya Jumanne wiki iliyopita Makonda alikabidhiwa ekari 1500 za ardhi na Mkurugenzi wa Azimio Housing Estate Mohamed Iqbal kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vigogo nchini, katika eneo la Kigamboni Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo eneo la Kisarawe II wilaya ya Kigamboni Mkurugenzi huyo alisema wameamua kumkabidhi eneo hilo ili kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuijenga Tanzania ya viwanda na kuwakomboa wananchi wenye uchumi wa kati.

Tuzo za Oscars zilivyozua Mgogoro

Tuzo za Oscars zimezua mgogoro baada ya mchanganyiko wa matokeo uwanjani.
Awali filamu ya kimuziki ya LALA Land ilitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hizo.
Lakini cha kushangaza ni kwamba baada ya waigizaji kupanda jukwaani na kusherekea ushindi ghafla mtangazaji alikuja na kutangaza upya.
Mtangazaji aliitangaza filamu ya Moonlight kuwa mshindi wa tuzo hizo.
Filamu ya Moonlight ni filamu inayosimulia hadithi ya mvulana mweusi anayeegemea mapenzi ya jinsia moja.
Hii ilileta purukushani katika hafla hiyo.

Mteule mwengine wa Trump akataa Uwaziri wa Jeshi la wanamaji

Mtu mwengine aliyeteuliwa na rais wa Marekani Donald Trump, kujaza wadhfa wa waziri wa jeshi la wanamaji amejiondoa baada ya kuonekana kukiuka sheria za taifa kuhusu mgongano wa maslahi.
Philip Bilden ameeleza wasiwasi wake kuhusu maisha yake ya usiri na changamoto alizokumbana nazo katika kujitenganisha na biashara zake.
Waziri wa usalama, Jim Mattis, amesema atampendekeza mtu atakayechukua nafasi ya Bilden katika kipindi cha siku chache zijazo.
Mteuliwa wa Rais Trump aliyependekezwa kusimamia jeshi la Marekani alijiondoa mapema mwezi huu.

Sunday, 26 February 2017

ZILIZOTAWALA KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEB 27 2017




Hafla ya kuapishwa kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Mabalozi

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Thobias Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Pindi Chana kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Silima Kombo Haji kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sudani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Abdallah Kilima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ikulu jijini Dar es Salaam.
6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Matilda Masuka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Ikulu jijini Dar es Salaam.
7
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu pamoja na Mabalozi Pindi Chana, Balozi Silima Kombo Haji, Abdallah Kilima pamoja na Balozi Matilda Masuka mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi (wapili kutoka kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba(Wakwanza kulia) , Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Hamad Masauni (Wakwanza kushoto) pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye(Watatu kutoka kushoto waliosimama mstari wa nyuma) na Mabalozi Pindi Chana(Wakwanza kulia walisimama mstari wa nyuma ) , Balozi Matilda Masuka(Wapili kutoka kulia waliosimama mstari wa nyuma), Balozi Abdallah Kilima(Wapili kutoka kushoto mstari wa nyuma) na Balozi Silima Kombo Haji (Wakwanza kushoto waliosimama) mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
WhatsApp Image 2017-02-26 at 13.22.25
WhatsApp Image 2017-02-26 at 13.22.02
WhatsApp Image 2017-02-26 at 13.25.18