Mlipuko mkubwa ulisikika karibu na uwanja huo wa ndege.
Duru kutoka jeshi la wanahewa la Saudia zimenukuliwa na shirika la utangazaji la serikali ya Al-Arabiya zikisema kombora hilo lilitunguliwa kaskazini mashariki mwa mji huo mkuu.
Runinga yenye uhusiano wa waasi wa Houthi kutoka yemen limesema kombora hilo lilikuwa limerushwa kulenga uwanja huo wa ndege.
Shirika la habari la serikali la Al-Ekhbariya limesema kombora hilo lilikuwa "ndogo kiasi" na kwamba hakuna uharibifu uliotokea.
Kombora hilo la masafa marefu lilikuwa limerushwa kulenga uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mfalme Khalid, kwa mujibu wa televisheni ya wapiganaji wa Houthi ya Al-Masirah.
Yemen imesambaratishwa na vita kati ya wanajeshi watiifu kwa serikali inayotambuliwa kimataifa ya Rais Abdrabbuh Mansour Hadi na wapiganaji wa kundi la waasi wa Houthi.
Saudi Arabia inaongoza kampeni ya kuwashinda wapiganaji hao wa Houthi.
No comments:
Post a Comment