Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha
Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf
Kallsting (wa pili kushoto) wakisaini Makubaliano ya Msaada wa jumla ya
Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango
wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James (kulia)na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na
Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting
(kushoto) wakisaini Makubaliano ya Msaada wa jumla ya Sh. bilioni 435.79
kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika
ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na
Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting
(kushoto) wakiwa wameinua juu Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh.
bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa
elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Maafisa waandamizi kutoka Ubalozi
wa Sweden Nchini Tanzania wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa
Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti
na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango, Bi Amina Khamis Shaaban (Kushoto), Kamishna Msaidizi
wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bi. Mamelta Mutagwaba na wengine
wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh.
bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa
elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msaada
wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kutoka Sweden kwa ajili ya Msaada wa
kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, ambapo amesema msaada huo unatoa
fursa kwa Serikali kupeleka fedha zilizotakiwa kutekeleza majukumu hayo
maeneo mengine ya Maendeleo ya Wananchi, hafla iliyofanyika Jijini Dar
es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na
Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting
(kushoto) wakibadilishana Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni
435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu,
katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha
Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf
Kallsting (wapili kulia) pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya
Fedha na Mipango na Ubalozi wa Sweden wakiwa katika Picha ya pamoja
baada ya kusainiwa Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79
kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika
ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango
Dares Salaam, Novemba 14, 2017:
Sweden imeipatia Tanzania Msaada wa jumla ya Fedha ya Sweden SEK.
Bilioni 1.64 ambayo ni sawa na takribani Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya
Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu.
Makubaliano ya msaada huo
yamesainiwa Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo
wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting.
Bw. James alisema kuwa imesainiwa
Mikataba mitatu ya msaada huo ambayo ni; mkataba kwa ajili kusaidia
Bajeti ya Serikali wa kiasi cha SEK milioni 600 ambazo ni sawa na Sh.
bilioni 159.59 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2017/18 hadi 2019/2020,
ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 watatoa takribani Sh. bilioni 53.20.
Alisema fedha hizo zitaelekezwa
katika kuboresha uhalisia wa Bajeti ili kuweza kutimiza majukumu ya
kisera, kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ya kikodi na yasiyo ya
kodi na pia kusaidia Serikali kutoa huduma nzuri kwa wananchi kupitia
taratibu za manunuzi.
Mkataba mwingine ni kwa ajili ya
kusaidia Mpango wa Elimu kwa Matokeo (EPforR) wa kiasi cha Fedha ya
Sweden SEK milioni 885 ambayo ni sawa na Sh. bilioni 235.40 kuanzia
mwaka 2017/18 hadi 2020/2021.
“Lengo la msaada huu ni kusaidia
Mpango wa Elimu kwa Matokeo ambapo tunapimwa namna ambavyo tumeweza
kutimiza wajibu wetu tuliojiwekea katika bajeti. Baada ya ya Serikali
kutimiza wajibu wake wa kupeleka fedha katika Sekta ya Elimu kwa wakati,
wameamua kutupatia fedha hizo ambazo Serikali tunazipangia kazi
kulingana na vipaumbele”, alieleza Bw. James.
Alieleza kuwa Mpango wa Elimu kwa
Matokeo ulianza mwaka 2015/ 2016 na katika kipindi hicho yamepatikana
maendeleo makubwa katika ujenzi wa miundombinu ya madarasa, vyoo,
mabweni. Utekelezaji wake umefanywa katika shule 361 kwenye Halmashauri
129 nchini.
“Katika Mpango huo Vyuo 17 vya
Walimu vimekarabatiwa ikiwa ni pamoja na kununua Kompyuta 260, Magodoro
6,730 na viti 1,976. Mpango huu unafanikiwa kutokana na dhamira ya
Serikali ya Awamu ya Tano ya kuweka mkazo katika Sekta ya Elimu hivyo
kupeleka fedha kwa wakati jambo linalosababisha washirika wa maendeleo
wazidi kutuamini” alifafanua Bw. James.
Mkataba wa tatu ni Marekebisho ya
Mkataba wa Mpango wa Kusoma, Kuhesabu na Kuandika ambao una kiasi cha
Dola za Marekani 94.8 zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Global Partnership for Education (GEP) na kukabidhiwa kwa nchi ya Sweden ili iweze kuusimamia.
Akifafanua kuhusu Mkataba huo Bw.
Doto James alisema kuwa Serikali ili saini Mkataba huo na Sweden Mei,
2015 na muda wa utoaji wa fedha hizo ulikwisha Agosti, 2016 na kubakia
kiasi cha Dola milioni 18.3 ambazo zitapatikana baada ya kusainiwa kwa
mkataba huo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo
cha Ushirikiano na Maendeleo katika Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania
Bw. Ulf Kallsting amesema kuwa nchi yake imedhamiria kuhakikisha
inajenga uwezo na ujuzi kwa watanzania kuanzia elimu ya Awali kwa kuwa
nchi yake inathamini sana elimu.
Bw. Kallsting alisema kuwa
Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Sweden na inatekeleza kwa ufanisi
miradi mbalimbali hivyo nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika
maeneo mbalimbali ya Maendeleo ili kufanikisha mipango yake.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bw. Doto James ameishukuru Sweden kwa niaba ya Serikali kwa
kuendelea kuisaidia Tanzania katika kutekeleza bajeti yake.
Imetolewa na;
Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
No comments:
Post a Comment