Mh. Jakaya Kikwete amekubali ombi hilo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo (SUA) kilichopo mkoani Morogoro, baada ya kutembelea chuoni hapo
akiwa na wataalamu wake wa mifugo kwa lengo la kujifunza mambo
mbalimbali kuhusu kilimo na mifugo.
Uongozi wa SUA ukatumia nfasi hiyo kuwasilisha ombi lao kwa Mh. Kikwete
ambaye alikubali na rasmi kuingia makubaliano ya pamoja ili kulitumia
shamba lake la mifugo kama shamba darasa la kutolea elimu ya vitendo kwa
wanafunzi wao, wataalamu wa mifugo na wafugaji.
Aidha Rais Mstaafu ameeleza kulizishwa na mafunzo aliyoyapata chuoni
hapo na kutoa ahadi ya kuendelea kushirikiana na chuo hicho kwa lengo la
kuleta mabadiliko ya kisayansi ya sekta ya ufugaji iweze kumletea tija
mfugaji.
Rais Mstaafu Kikwete kwa sasa amejikita zaidi kwenye suala la ufugaji wa
kisasa wa ng’ombe wa maziwa, kilimo cha mazao ya chakula na matunda
hasa mananasi kijijini Msoga, Chalinze , wilayani Bagamoyo, mkoa wa
Pwani.
No comments:
Post a Comment