Waziri Mwakeyembe ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wageni waliofika kwenye uzinduzi wa television mpya ya Jasson, ambayo itakuwa inaonyesha kazi za sanaa za Tanzania, na kuwataka wasani wa Tanzania kutumia viu vya kitanzania ili kutangaza Utanzania na kuwa na maudhui ya Mtanzania.
"Soundtrack hakuna sababu kwa nchi tajiri kwa muziki kama Tanzania kwa msanii wa Kinyakyusa, msanii wa Kimakonde kutumia soundtrack eti za kizungu, ashakhum si matusi huo ni ushamba kwa kweli, ni matarajio ya wizara baada ya miaka kadhaa mtu akisikia soundtrack ya , Mdumange, Mganda, Sindimba ajue anaangalia filamu ya Tanzania", amesema Waziri Mwakyembe.
Pamoja na hayo Waziri Mwakyembe amewataka wasanii hao kuzingatia matumizi ya lugha ya Kiswahili, ambayo kwa sasa inatambulika zaidi duniani.
No comments:
Post a Comment