Friday, 17 November 2017

Ndege ya Kuwait yakataa kumbeba raia wa Israel


Mahakama nchini Ujerumani imeamua kuwa shirika la ndege la Kuwait lilikuwa na haki ya kukataa kumbeba raia wa Israel.
Uamuzi huo imegawadhabisha makundi ya wayahudi wanaosema kuwa unahalalisha ubaguzi dhidi ya wayahudi.
Shirika la ndege la Kuwait lilifuta tiketi ya abiria hiyo kutoka Frankfurt kwenda Bangkok.
Mahakama ya Frankfurt ilisema kuwa shirika hilo lilikuwa linafuata sheria za Kuwait amabzo hazitambui taifa la Israel.
Ilisema haikuwa na uwezo wa kuamua kuhusu sheria ya Kuwait na kuwa sheria za Ujerumani zinaamua katika masuala kuhusu ukabila, dini lakini sio kwa uraia.
  • UN yainyooshea kidole Israel
  • Israel kudhibiti mipaka yake
  • Kanisa takatifu lafunguliwa Israel
Nathan Getlbart, wakili wa abiria huyo aliutaja uamuzi huo wa mahakama kama pigo kwa demokrasia na kwa Ujerumani kwa ujumla.
Baraza la wayahudi nchini Ujerumani lilisema kuwa ni jambo lisilokubalika kuwa kampuni ya kigeni inayofanya kazi kwa misingi ya ubaguzi dhidi ya wayahudi, itaruhusiwa kufanya biashara nchini Ujerumani.



"Tunaiomba serikali kuhakikisha kuwa visa kama hivyo havitokei siku usoni," alisema meya ya Frankfurt Uwe Bekcer.

No comments:

Post a Comment