Dortmund italazimika kumuuza Aubameyang ili kuepuka hasara ya kuondoka bure kwa mchezaji huyo, haya yanakuja baada ya timu hiyo kutoka sare ya mabao 4-4 katika mchezo wao wa derby dhidi ya Schalke katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani.
Mara baada ya mchezo huo meneja wa kikosi hicho, Peter Bosz amesema kufuatia utovu wa nidhamu unaoonyeshwa na straika huyo wa kimataifa wa Gabon muda wa kubaki ndani ya klabu hiyo umekwisha.
Mlinda lango wa Dortmund, Roman Weidenfeller amesema meneja wa kikosi hicho, kachoshwa na ujinga unaofanywa straika huyo nakusema kuwa amepoteza kilakitu.
Liverpool na Chelsea ni klabu mbili ambazo zimeonesha nia za kutaka kumsajili mshambuliaji huyo.
No comments:
Post a Comment