Sethi na Rugemarila kusota Rumande mpaka Disemba 8 Mwaka huu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo ijumaa Novemba 24 2017, imeahirisha
kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme
ya IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara, James Rugemarila hadi
Desemba 8, 2017, kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.
Upande wa mashtaka umemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa
wanaomba upelelezi ukamilike kwa haraka kwasababu hali ya mshtakiwa
mmoja si nzuri.
Harbinder Singh Sethi pamoja na Mfanyabiashara James Rugemarila, kwa
pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya kutakatisha fedha na
kuisababisha Serikali hasara ya zaidi ya Bilioni 3.
No comments:
Post a Comment