Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo alipoenda kutembelea meli yenye madaktari bingwa kutoka China ambayo imetia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam, na kutoa huduma za vipimo na matibabu kwa wakazi wa Dar es salaam bila gharama yoyote.
"Tunapenda kusema shukrani kwa dhati kwa serikali ya China kuamua kuituma meli na madaktari kuja Tanzania, tunafurahi kwa huduma zao, wameokoa maisha ya watanzania zaidi ya elfu 6,400, huu ni upendo wa pekee unaogusa, ndio maana leo nimeshindwa kuvumilia nimeona bora nije nishukuru, nimeguswa mno na ndugu zetu wachina, yapo mataifa mengine matajiri, yenye mali nyingi lakini hayajaguswa", amesema Rais Magufuli.
Sambamba na hayo Rais Magufuli amewakabidhi madaktari hao barua maalum kwenda kwa raisi wa nchi yao Xi Jinping pamoja na kinyago kama zawadi kwake, kumshukuru kwa mchango wake na ukarimu wake kwa watanzania masikini.
Pia Rasi Magufuli amewatakia safari njema madaktari hao na kuwaomba kurudi tena wakati mwengine, na kuwataka kukaa kwa muda mrefu zaidi ili waweze kutoa huduma kwa watanzania wengi hata watakaotoka mikoani.
No comments:
Post a Comment