Mkurugenzi wa vipindi na
uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba leo amemzungumzia Zamaradi
Mketema ambaye alikuwa mpenzi wake, mahusiano yao yaliweza kudumu kwa
muda kiasi cha kutoa matunda ya watoto wawili (2) kwa mujibu wa maelezo
ya Ruge.
Akiwa kwenye mahojiano Clouds TV
kupitia kipindi cha asubuhi CLOUDS 360 Runge amefunguka kama ifuatavyo
baada ya kuulizwa maswali yafuatayo: 1. Je ulikuwa unajua kama Zamaradi
anaelekea kufunga ndoa? 2. Ile sauti niyakwako?
RUGE: “Kila kilicho fanyika nilikuwa na
taarifa nacho na ninakipa baraka asilimia mia moja 100%, kwa sababu
hii ni sehemu ya maisha tunapita. Kubwa kuliko yote nina watoto wawili
(2) ambao nimezaa na Zamaradi Mketema namuheshimu mmno mpaka sasa
naendelea kumuheshimu kama Mama watoto wangu. Naheshimu na kuwapenda
sana watoto wangu na nimewaona weekend iliyopita so heshima inatakiwa
iwepo”.
No comments:
Post a Comment