Waziri Mpina ameagiza wawekezaji hao kulipa malimbikizo yote ya madeni ya Serikali ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.
Miongoni mwa kampuni zinazoathiriwa na maamuzi hayo Overland iliyokuwa imeingia ubia wa hisa kwa asilimia 70 na kubakiza asilimia 30 ya hisa kwa Narco kwa ajili ya kuwekeza mifugo na kujenga miundombinu muhimu katika Ranchi ya Mkata lakini mkataba huo umeonekana kutokuwa na maslahi yoyote kwa Taifa huku kukiwa hakuna uwekezaji wowote uliofanywa.
Waziri Mpina amefikia uamuzi huo leo Jumamosi baada ya kutembelea ranchi hizo na kukagua mikataba pamoja na maeneo hayo na kusema katika mkataba wa Overland na Narco umeonekana kuikosesha Serikali mapato ya kutosha kutokana na thamani ya ardhi yenye ukubwa wa hekta 19,000 na miundombinu iliyopo hivyo ugawaji wa hisa haujawa na masilahi kwa Taifa na kwamba tangu mkataba huo uliposainiwa mwaka 2015 hadi sasa hakuna uwekezaji wowote uliofanyika.
Waziri Mpina ameagiza Narco kuvunja mikataba ya mwekezaji Kadoro Farm Company Limited mwenye kitalu namba 418, Bagamoyo Farm mwenye kitalu namba 419, A to Z animal feeds Company Limited mwenye kitalu namba 420 na Ereto Livestock Keepers Association mwenye kitalu namba 422 kutokana na kushindwa kuendeleza mashamba yao zaidi ya miaka 10 tangu walipomilikishwa mwaka 2007 na hawalipi kodi ya Sh 1,000 kwa ekari kwa mwaka hivyo.
Waziri ameagiza walipe malimbikizo ya madeni yao ndani ya mwezi mmoja na mkataba wao uvunjwe.
No comments:
Post a Comment